Villarreal kuvizia Liverpool
NA MASHIRIKA
MERSEYSIDE, Uingereza
LIVERPOOL wako nyumbani ugani Anfield leo usiku kuwakaribisha Villarreal katika mechi ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, hatua ya Nne Bora.
Jumanne usiku, Real Madrid walipepetana na wenyeji Manchester ugani Etihad na matokeo yakawa 4-3 kwa faida ya wenyeji.
Tayari mashabiki wengi wanabashiriki uwezekano wa fainali ya Waiingereza watupu – Liverpool na Manchester City – kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo Chelsea waliichapa Manchester City 1-0 na kutwaa ubingwa.
Vile vile kuna wale wanaotarajia fainali ya wababe wawili wa Uhispania- Madrid na Villarreal ambao wameweka historia ya kulaza vigogo kwenye michuano hiyo msimu huu.
Villarreal ambao ndio mabingwa wa Europa League wananolewa na kocha Unai Emery ambayo anakaribia kufikia mafanikio ya FC Porto ilipokuwa chini ya Jose Mourinho na kunyakua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2003/04 baada ya kushinda Kombe la Europa.
Msimu huu, Villarreal iliwabandua Juventus katika hatua ya 16-Bora kabla ya kushangaza wengi kwa kuwatupa nje Bayern Munich kwenye robo-fainali na kufuzu kwa nusu-fainali ambapo kibarua kiliyopo mbele yao ni kushinda Liverpool na kufuzu kwa fainali.
Ni timu inayojivunia mastaa kadhaa, lakini huenda mambo yakawa magumu ugani Anfield mbele ya mashabiki wengi wa The Reds.
Kwenye msimu wa 2015/16 Villareal walishinda Liverpool 1-0 katika mkondo wa kwanza wa nusu-fainali ya Europa League, lakini wakacharazwa 3-0 katika mechi ya marudiano pale Anfield na kusonga mbele.
Tayari kocha Jurgen Klopp amesema mechi hii itakuwa ngumu na kila timu itahitaji umakinifu hadi dakika ya mwisho.
Wakati huo huo, Manchester City wamekanusha madai ya kumnyemelea Paul Pogba wa Manchester United.
Mkataba wa kiungo huyo pale Old Trafford unamalizika mwishoni mwa mwezi Juni, ambapo atakuwa huru kuondoka kama mchezaji huru.
Juventus, Real Madrid na Paris Saint-Germain ndizo timu pekee zilizoonyesha nia ya kumtaka Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 29, lakini uvumi wa hivi punde umedai kwamba anajiandaa kujiunga na City.
Kocha Pep Guardiolaamesisitiza kwamba aliwahi kumkataa nyota huyo mnamo 2018 wakati Jose Mourinho akiwa kocha wa Manchester United.
Kudfikia sasa, Pogba amefunga bao moja pekee na kutoa pasi 27 msimu huu, wakati anaendelea kusumbuliwa na jerah la pajani.
Next article
TAHARIRI: Wawaniaji urais watumie vyema fursa hii ambayo…