[ad_1]
Maambukizi ya Covid yaanza kupanda tena
CHARLES WASONGA na PSCU
IDADI ya maambukizi ya Covid-19 nchini imeanza kupanda tena huku watu 82 zaidi Jumapili wakithibitishwa kuambukizwa kutokana na sampuli 2,197 kupimwa.
Mnamo Jumamosi, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe aliripoti kiwango cha maambukizi cha asilimia 5.6.
Hiki kilikuwa kiwango cha juu zaidi kuandikishwa nchini tangu Machi 11, 2022 serikali ilipolegeza masharti ya kuzuia maambukizi ya Covid-19, ikiwemo kuvalia barakoa katika maeneo ya umma.
Ongezeko la visa vya maambukizi limeibua hofu ya kutokea kwa wimbi la sita la nchini.
Hata hivyo, wataalamu wa afya wamepuuzilia mbali hofu hiyo wakisema hali hiyo haitatokea kwa sababu wananchi wengi wamejenga kinga miilini mwao.
Wataalamu wanasema ongezeko la maambukizi ya sasa linachangiwa na kusambaa kwa homa inayosababishwa na virusi vinavyofanana na vile vya corona.
[ad_2]
Source link