Connect with us

General News

Abiria 60 waponea chupuchupu ndege yao ikipoteza mwelekeo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Abiria 60 waponea chupuchupu ndege yao ikipoteza mwelekeo – Taifa Leo

Abiria 60 waponea chupuchupu ndege yao ikipoteza mwelekeo

NA DAILY MONITOR

ENTEBBE, UGANDA

ABIRIA 60, wakiwemo wanawake 20 kutoka Rwanda waliokuwa wakihudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mwana wa Rais Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, Jumatano asubuhi waliponea chupuchupu baada ya ndege kupoteza mwelekeo ilipokuwa ikitua katika uwanja wa Entebbe.

Ndege hiyo ya Shirika la RwandAir ilitua katika uwanja huo kutoka Nairobi lakini ikapoteza mwelekeo wakati wa kutua.

Wanawake 20, akiwemo mshindi wa zamani wa taji la urembo nchini Rwanda, Jolly Mutetsi, walikuwa wamealikwa kuhudhuria sherehe ya kuadhimisha miaka 48 ya Luteni Jenerali Muhoozi ambayo itafanyika Jumapili.

Katika taarifa, shirika la RwandAir lilisema tukio hilo “lilitokana na hali mbaya ya hewa”.

Abiria wote na wafanyakazi wa ndege walishuka salama bila majeraha yoyote, liliongeza.

Jenerali Muhoozi, ambaye pia ni kamanda wa majeshi ya nchi kavu, alichapisha ujumbe mtandaoni Jumatatu akithibitisha kuwa Mutetsi ni miongoni mwa wageni ambao watahudhuria sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending