Connect with us

General News

Achani ataka wapinzani wake kutoendeleza siasa za ukabila – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Achani ataka wapinzani wake kutoendeleza siasa za ukabila – Taifa Leo

Achani ataka wapinzani wake kutoendeleza siasa za ukabila

NA SIAGO CECE

NAIBU Gavana wa Kwale Fatuma Achani amewataka wapinzani wake kutoendeleza siasa za ukabila huku wakiwania kiti hicho cha ugavana Kwale.

Alieleza kuwa siasa hizo zinaleta mgawanyiko pia kwa misingi ya jinsia na dini.

“Hakuna haja ya watu kutia ukabila au dini katika siasa kwa sababu hii itatenganisha Wakwale ambao wana umoja. Muhimu ni kuuza sera zako kwa wapiga kura,” Bi Achani alisema.

Alikuwa akiongea Jumamosi katika hafla ya kutawazwa na familia na jamii yake huko Tiwi ili kuwa kiongozi.

Kutawazwa kwake kumekuja siku chache tu baada ya Bi Achani kupewa tikiti ya moja Kwa moja na chama cha United Democratic Alliance (UDA) kuwania ugavana wa Kwale mwezi Agosti mwaka huu.

Bi Achani , ndiye mwanamke pekee anayewania kiti cha ugavana Kwale. Wapinzani wake ni Profesa Hamadi Boga (ODM), Sammy Ruwa (PAA), Gereza Dena (KANU), Ali Chirau Mwakwere (Wiper) na Lung’anzi Chai.

Haya yanajiri huku Bi Achani akipigiwa debe na Gavana Salim Mvurya ambaye angependa naibu wake kumrithi.

Bw Mvurya ambaye alihudhuria sherehe hiyo aliwarai wakazi wa Kwale kumpigia kura Bi Achani na Naibu Rais William Ruto kama rais.

“Tutapigia Fatuma Achani kama gavana wetu, na kwa upande wa Rais, si mwingine bali ni Dkt William Ruto,” Bw Mvurya alisema.

Aliongeza kuwa mchujo wa UDA umefaulu nchini kwani hakuna chama kingine kilochofanya zoezi kama hilo.

Alisema kuwa ni kawaida kwa baadhi ya wanachama kutoa malalamishi kuhusu uchaguzi wa mchujo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending