Ghasia zilizuka Lesson Juni 25 baada ya polisi kumpiga risasi Lazarus Tirop. Picha: The Star. Source: UGC
Mahakama iliarifiwa kwamba Onyango alimuua Tirop Juni 25 alipojaribu kutatua mabishano yaliyozuka baada ya afisa huyo kumuitisha mhudumu wa bodaboda KSh 50 kwa kutovalia mski.
Ripoti zilisema konstebo huyo alifanyiwa uchunguzi wa kiakili na kupimwa dhidi ya COVID-19 kabla ya kufikishwa mahakamani.
Wakili wa Onyango Judy Muriuki aliiomba mahakama kumwachilia mshukiwa kwa dhamana na ombi hilo hilo litasikizwa Ijumaa, Julai 17.
Wakazi wenye ghadhabu waliiteketeza nyumba ya afisa huyo. Picha: The Star. Source: UGC
Mshukiwa Onyango atasalia katika kituo cha polisi cha Eldoret West.
Awali TUKO.co.ke iliripoti kuwa marehemu, ambaye alifanya kazi ya kushona viatu na kupaka rangi huko Lessos alijaribu kutatua mzozo baina ya afisa huyo na mhudumu wa boda boda.
Inadaiwa kwamba afisa huyo alikuwa akiitisha rushwa ya KSh 50 kutoka kwa mhudumu huyo baada ya kumpata bila maski.
Mhudumu huyo hata hivyo alianza kumsihi afisa huyo kumwachilia na ndiposa marehemu alipata kuvutiwa na mzozo wa wawili hao.
Katika hali hiyo mabishano makali yaliiibuka kati ya watatu hao na ndiposa afisa huyo akachomoa bunduki yake na kumfyatulia risasi mshonaji viatu huyo kichwani.
Wakazi waliposikia kilichotokea walipandwa na mori na kuanza kuchoma magurumudumu wakiandamana barabarani wakitaka mwathiriwa kutendewa haki.