[ad_1]
Afueni kuu kwa wakazi hospitali ikikamilika baada ya miaka 27
NA KNA
WAKAZI wa Rongai, Kaunti ya Nakuru wamejawa na furaha baada ya kupata kituo kipya cha afya walichokisubiri kwa muda wa miaka 27.
Kituo cha Afya cha Rongai-Turi kilianzishwa na serikali ya Rais Mwai Kibaki na kilidhamiriwa kuwa kituo bora zaidi katika maeneo ya mbali ya Wadi ya Mosop.
“Tunatoa wito kwa umma kutumia fursa hii ambapo huduma maalum za kiafya zinatolewa bila malipo au kwa ada ya chini,” alisema Gavana Lee Kinyanjui.
“Tuna matumaini kwamba siku za usoni kituo hiki pia kitatoa huduma za kusafisha damu, matumizi ya matibabu kimitambo, kifua kikuu, huduma za mochari na upasuaji wa miili, matibabu ya viini, kutibu saratani na huduma za upelelezi,” akaongeza wakati wa ufunguzi rasmi.
[ad_2]
Source link