Aliyekuwa mpenzi wa mrithi wa kampuni ya mvinyo ya Keroche Tecra Muigai anatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa kiakili kabla ya kujibu mashtaka ya mauaji dhidi yake
Omar Lali alipatikana na hatia ya kumuua marehemu Tecra mwezi Mei mwaka huu.
Jaji Roselyn Korir alisema Jumanne, Julai 14 kuwa mshukiwa afanyiwa ukaguzi wa kiakili katika hospitali ya rufaa ya Garissa.
Lali ambaye kwa sasa amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Garsen atafikishwa mahakamani Alhamisi, Julai 16 kujibu mashtaka kama alivyoamru hakimu mkuu wa mahakama ya Lamu Allan Temba.
Kulingana na uchunguzi wa maafisa wa polisi, Lali anasalia kuwa mshukiwa mkuu wa mauaji ya marehemu Tecra.
Kulingana na uchunguzi wa maafisa wa polisi, Lali anasalia kuwa mshukiwa mkuu wa mauaji ya marehemu Tecra. Source: UGC