Connect with us

General News

Aliyenajisi watoto sasa atabaki jela kwa miaka 46 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Aliyenajisi watoto sasa atabaki jela kwa miaka 46 – Taifa Leo

Aliyenajisi watoto sasa atabaki jela kwa miaka 46

NA BRIAN OCHARO

MWANAUME wa umri wa miaka 37 amefungwa jela miaka 46 kwa kunajisi watoto wawili mwaka 2012.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Mombasa Ann Ong’injo alikataa kumwachilia Swaleh Mwinyi, akamfunga jela miaka 46 badala ya kifungo cha maisha ambacho alikuwa amepewa awali na korti ya chini.

Mwinyi aliwadhulumu watoto hao mtaani Kaloleni kati ya Aprili 13 na Oktoba 14, 2012.

“Kwa kuzingatia mwenendo wa sasa unahitaji hukumu maalum kupewa mfungwa, narekebisha adhabu hiyo kwa kumpa Mwinyi kifungo cha miaka 23 jela kwa kila shtaka. Hukumu hii itaenda sambamba,” alisema Jaji.

Mashtaka yalihibitisha kuwa Mwinyi aliwanyanyasa kingono watoto hao katika mtaa wa Kaloleni eneo la Mvita kati ya Aprili 13 na Oktoba 14, 2012.

Watoto hao waliambia mahakama kuwa walipokuwa wakielekea shuleni asubuhi, Mwinyi angewapa dawa za kulevya kabla ya kuwanajisi.

Wakati fulani angefanya hivyo jioni.

“Alikuwa ananichafua asubuhi sana ninapoenda shuleni au ninaporejea nyumbani,” mtoto huyo aliambia mahakama wakati wa kesi ya Bw Mwinyi.

Kulingana na watoto hao, Mwinyi alikuwa akiwanunulia zawadi kama Milo Chocolate, mabuyu, peremende na wakati mwingine alikuwa akiwapa pesa.

Alikuwa akiwangojea njiani asubuhi au jioni.

Rekodi za matibabu zilithibitisha kuwa watoto hao walikuwa wamenajisiwa na mshukiwa.

Kutokana na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka, Mwinyi alipatikana na hatia ya kuwanajisi wsichana hao na kuhukumiwa kutumikia kifungo cha maisha gerezani.

Hata hivyo, Bw Mwinyi hakuridhishwa na hukumu hiyo na akapendelea kukata rufaa kwa Mahakama ya Kuu.

Hapo alilalamikia hukumu hiyo kuwa kali mno huku akiikosea mahakama ya mahakimu kwa kumpata na hatia kutokana na ushahidi uliogubikwa na utata.