Connect with us

General News

Aliyetolewa Mto Yala aliuawa kwa kugongwa kichwani – Ripoti – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Aliyetolewa Mto Yala aliuawa kwa kugongwa kichwani – Ripoti – Taifa Leo

Aliyetolewa Mto Yala aliuawa kwa kugongwa kichwani – Ripoti

NA STEPHEN MUNYIRI

MWANAMUME wa Kaunti ya Nyeri ambaye mwili wake ni miongoni mwa ile iliyoopolewa kutoka Mto Yala, huenda aliuawa kwa kugongwa kichwani na kifaa butu kabla maiti yake kutupwa mtoni, ripoti ya upasuaji maiti imefichua.

John Kiruki Karimi aliyekuwa na umri wa miaka 28 na ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Ngurumo katika Kaunti Ndogo ya Mathira Magharibi, alitoweka Novemba 2021 akiwa safarini kutoka mtaa wa Umoja 3 jijini Nairobi kuelekea Nakuru.

Kulingana na familia yake, ripoti ya upasuaji wa mwili uliofanyiwa katika hospitali ya Siaya, ilionyesha kuwa marehemu aligongwa na kifaa butu kabla ya kufariki na mwili wake kutupwa kwenye mto huo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending