Connect with us

General News

Ashuu ashusha pumzi kwa muda – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ashuu ashusha pumzi kwa muda – Taifa Leo

Ashuu ashusha pumzi kwa muda

NA BRIAN OCHARO

JOPOKAZI la kutatua mizozo ya vyama vya kisiasa limesimamisha kwa muda uamuzi wa chama cha ODM kumteua Bi Zamzam Mohamed kuwania nafasi ya Mwakilishi wa Kike Mombasa.

Uamuzi huo umetolewa kufuatia malalamishi ya mpinzani wake, Bi Asha Hussein Mohamed almaarufu ‘Ashuu’, ambaye amedai hakutendewa haki. Mwanachama wa jopokazi hilo, Bw Erastus Orina, alisema uamuzi huo utadumu hadi maagizo zaidi yatakapotolewa.

Chama kilifanya kura za mchujo mnamo Aprili 22, ambapo Bi Zamzam alitangazwa mshindi.