Connect with us

General News

Aubameyang abeba Barcelona dhidi ya Real Sociedad ligini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Aubameyang abeba Barcelona dhidi ya Real Sociedad ligini – Taifa Leo

Aubameyang abeba Barcelona dhidi ya Real Sociedad ligini

Na MASHIRIKA

BAO la tisa la fowadi Pierre-Emerick Aubameyang kutoka na mechi 11 katika kampeni za Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) liliwezesha Barcelona kusajili ushindi wa 1-0 dhidi ya Real Sociedad na kupaa hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa jedwali mnamo Alhamisi usiku.

Nyota huyo wa zamani wa Arsenal alicheka na nyavu za Sociedad kunako dakika ya 11 baada ya kushirikiana vilivyo na kiungo wa zamani wa Manchester City, Ferran Torres.

Nusura Sociedad wasawazishe mwishoni mwa kipindi cha kwanza ila juhudi za wavamizi Alexander Sorloth na Alexander Isak zikazimwa na kipa Marc-Andre ter Stegen. Aubameyang alipachika wavuni bao lake dakika chache baada ya kombora la Ousmane Dembele kugonga mwamba wa goli la Sociedad.

Mechi hiyo ilisimamishwa kwa muda mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya mashabiki kuanza kurusha vifaa uwanjani.

Aubameyang, 32, aliingia katika sajili rasmi ya Barcelona bila ada yoyote mnamo Februari 2022. Hiyo ilikuwa baada ya kuvuliwa unahodha wa Arsenal mnamo Disemba 2021 kutokana na utovu wa nidhamu.

Ni Memphis Depay ambaye amefungia Barcelona idadi kubwa ya mabao katika La Liga msimu huu kuliko Aubameyang. Ushindi dhidi ya Sociedad ulipaisha Barcelona hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa jedwali la La Liga kwa pointi 63 japo pengo la alama 15 linatamalaki kati yao na viongozi Real Madrid.

Sociedad kwa upande wao walisalia katika nafasi ya sita jedwalini kwa alama 55, sita nyuma ya mabingwa watetezi Atletico Madrid wanaofunga orodha ya nne-bora. Zimesalia mechi tano pekee kabla ya kampeni za La Liga msimu huu kutamatika rasmi.

Real wanahitaji alama nne pekee kutokana na mechi tano zilizosalia ligini muhula huu ili kunyanyua taji la La Liga kwa mara ya 35 katika historia.

MATOKEO YA LA LIGA (Alhamisi):

Sociedad 0-1 Barcelona

Espanyol 0-1 Vallecano

Levante 2-3 Sevilla

Cadiz 2-3 Bilbao

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending