Connect with us

General News

Avutiwa kwa filamu na kipindi cha ‘Pete’ – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Na JOHN KIMWERE

PENYE nia pana njia. Ndivyo wahenga walivyologa, tangia zama zile baada ya kupasua hilo mpaka sasa, msemo huo ungali na mashiko siyo haba miongoni mwa jamii kwa jumla.

Isabellah Mlagala ameorodheshwa miongoni mwa wasanii chipukizi wanaojiwekea matamanio ya kutinga upeo wa kimataaifa miaka ijayo.

Hata hivyo binti huyu mwenye umbo la kuvutia ambaye kwa jina la msimbo anafahamika kama Dettah kando na uigizaji amehitimu kama mwalimu wa shule za msingi.

”Kando na Dettah pia ninajulikana kwa majina mengine tofauti kama Tunu, Elizabeth na Taiyo kulingana na filamu nilizowashiriki,” anasema na kuongeza kuwa alivutiwa na uigizaji tangia akisoma kidato cha pili.

Msichana huyu alivutiwa na uigizaji baada ya kutazama kipindi cha ‘Pete’ ambacho hupeperushwa kupitia runinga ya Maisha Magic. Anasema kuwa anatamani sana kufikia hadhi ya msanii Aisha Mwajuma ambaye ni kati ya walioshiriki kipindi hicho cha Pete.

Chipukizi huyu amefanya kazi na makundi mbali mbali ikiwamo Nairobi Theatre, Foever Arts Production, Planets Production na Five Star Production.

Binti huyu ambaye hajapata mashiko zaidi katika tasnia ya maigizo anajivunia kushiriki kipindi kiitwacho Sumu kilichopeperushwa kupitia runinga ya Raia TV mwaka 2017. Aidha aliwahi kushiriki kipindi kwa jina ‘Salome’ kilichopeperushwa kupitia runinga ya KBC.

Kwa waigizaji wa humu nchini anasema angependa sana kutua jukwaa moja na wenzake ambao hushiriki kipindi cha ‘Pete’ na ‘Kina’ Aisha Mwajuma’ na Sanaipei mtawalia.

Avutiwa kwa filamu na kipindi cha ‘Pete’ – Taifa Leo

Katika Ukanda wa Afrika Mashariki anasema angependa kufanya kazi na Grace Mapunda mzawa wa Tanzania ambaye ameshiriki kipindi cha Huba ambacho huonyeshwa Maisha Magic.

Katika mpango mzima anasema kwake uigizaji ni ajira ambapo nyakati zote anapopata nafasi hushiriki kwa kujitolea. Hayo kando anapiga hesabu ya kuanzisha brandi yake ndani ya miaka mitano ijayo.

Kipusa huyu aliyezaliwa mwaka 2000 anasema serikali inastahili kuunga mkono sekta ya uigizaji kikamilifu kupitia kutega fedha za kuwapiga jeki waigizaji wanaokuja wavulana kwa wasichana.

”Kusema ukweli taifa hili limefurika waigizaji wengi tu lakini wanahitaji kushikwa mikono kwa njia mbali mbali ili kutimiza maazimio yao. Wenzetu waliotangulia wanapaswa kuwa mstari wa kwanza kutuonyesha mwelekeo lakini baadhi yao hupenda kutubomoa na kujitakia makuu,” akasema.

Kiukweli waigizaji wapya kwenye gemu hupitia pandashuka nyingi. ”Kama hauwezi kufuata saa vizuri inakuwa rahisi kupoteza nafasi ya ajira. Pia kudhalilishwa na maprodusa wakiume bila kuweka katika kaburi la sahau kuambiwa hatuwezi kufika mahali kisanaa,” akasema.

Pia anashauri wenzie kuwa ulimwengu wa sasa unahitaji wawe wabunifu ili kupiga chenga matatizo ya kukosa ajira. Anasema uigizaji sio jambo rahisi pia sio kulazimisha lazima muhusika awe na mapenzi ya kushiriki kutoka moyoni.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending