Mtangazaji Grace Msalame ametangaza rasmi kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni mjamzito, ujmbe ambao umepokelewa vema na mashabiki wake
Mama huyu wa mapacha wawili alipakia picha kwenye Instagram akimshukuru Mungu kwa kubariki tumbo lake la uzazi kwa mara nyingine.
Grace Msalame tayari yuko na mapacha wawili wa kike
Msalame alifichua kuwa licha ya kupitia changa moto za hapa na pale ikiwemo kusumbuliwa na ugonjwa wa fibroids, anamshukuru Mungu kwani kwa sasa ana ujauzito wa miezi sita.
” Miezi sita baadaye, ishara zishaanza kuonyesha, tumbo yangu sasa imekuwa kubwa, nasubiri kwa hamu kuwa mama wa watoto watatu,” Alisema Msalame.
Mashabiki wake na marafiki wa karibu akiwemo aliyekuwa mtangazji wa Citizen TV, Terryanne Chebet, Awinja na wengine wengi wamempongeza na kumtakia heri njema.

Grace Msalame
“Mungu ni mwaminifu, sikuwahi jua kwamba siku moja nitafika hapa nilipo lakini ona makuu ambayo Mungu amenifanyia, licha ya kusumbuliwa na Fibroids miaka miwili iliyopita sasa naweza kutabasamu kwani ameyajibu maombi yangu,” Alimjibu mmoja wa mashabiki wake.
Msalame alikuwa ameolewa na Paul Ndichu, pacha wa mumewe mtangazaji wa zamani wa Citizen TV Janet Mbugua, Eddie Ndichu ila ndoa yao ikavunjika na wakaamua kutengana.
Kwa pamoja Msalame na Ndichu wamejaliwa mapacha wawilili wa kike.