Connect with us

General News

Baadhi ya takwimu za kurejelea mafanikio ya Jubilee zatiliwa shaka – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Baadhi ya takwimu za kurejelea mafanikio ya Jubilee zatiliwa shaka – Taifa Leo

Baadhi ya takwimu za kurejelea mafanikio ya Jubilee zatiliwa shaka

NA MWANGI MUIRURI

WASHAURI na wanaomwandikia Rais Uhuru Kenyatta hotuba zake za kusomewa umma wamesutwa kama ambao humfanya ajiangazie kama ‘mwongo’ kuhusu hali halisi ya kiuchumi na pia kisiasa nchini.

Huku rais akiwasisitizia Wakenya kwamba serikali yake imefanya makubwa katika kuimarisha bei za bidhaa za kilimo, kudhibiti uchumi hadi ukapanuka kutoka Sh5 trilioni mwaka 2012 hadi Sh13 trilioni za sasa na pia kupunguza bei za vifaa na pembejeo za kilimo, wadau wanasema maelezo hayo hayaafiki hali halisi.

Anakumbushwa kuwa kati ya uchumi huo wa Sh13 trilioni, bunge liliipa serikali yake idhini ya kukopa hadi Sh12 trilioni na ambapo hadi sasa imekopa Sh8 trilioni ambazo riba ni Sh3 trilioni na pengo au nakisi ya bajeti ya 2022/23 ikitarajiwa kuzidi Sh1 trilioni.

Aidha, deni kwa wanakandarasi nalo linatarajiwa kutinga Sh1 trilioni, kumaanisha uchumi umejengwa juu ya madeni ambayo yanaweza yakasababisha taifa kupigwa mnada.

“Ukweli ambao rais hutoa na ambao haupingiki ni kuhusu ujenzi wa barabara mashinani. Hata wanaompinga kabisa watajiangazia kama wafitini ikiwa watasema serikali yake haijajenga barabara. Lakini katika masuala mengine, rais huwa anaaibishwa hadharani na wanaomshauri kusoma takwimu zake,” asema Joseph Murugi ambaye ni Mkurugenzi wa utafiti katika Taasisi ya Masomo kuhusu Bajeti na Ugatuzi nchini (CB&DS).

Bw Murugi anasema kuwa rais husema vile serikali yake imeunganisha watu na umeme na pia maji safi huku ikiwa wazi kwamba gharama ya bidhaa hizo mbili muhimu iko juu sana kiasi cha kutatiza na kudidimiza faida katika uzalishaji.

“Hali nyingine ambayo rais huwa anatukanganya akisema ameimarisha ni kuhusu mageuzi katika sekta ya majani chai. Tulisisimka sana kuona Shirika la Majani Chai Ncini (KTDA) likivunjwa na chaguzi kuandaliwa huku tukiahidiwa pato lililoimarika kwa asilimia 60. Lakini hadi sasa, kilo moja ya majani chai inalipwa kwa ile bei ya zamani ya Sh21 huku bonasi ikiwa ni ile ile ya Sh10. Kile tu kimebadilika ni kwamba tangu mabadiliko hayo yaletwe, tunalipwa mapema,” asema Bw Mugwe Njunu ambaye ni mshirikishi wa vuguvugu la kutetea haki za wakulima wa chai Mlima Kenya.

Huku rais akisisitiza kwamba bei ya kahawa imeimarika hadi Sh110 kwa kilo moja, mwenyekiti wa wakulima wadogowadogo katika ukanda wa Mlima Kenya James Miriti anasema kuwa hali hiyo si sahihi.

“Cha kuelewa ni kwamba hakuna wakati bei ya kahawa itawiana kitaifa kwa kuwa malipo huzingatia ubora, uwajibikaji wa wasimamizi wa mashirika, bei katika mnada na pia ada za benki inayolipa mkulima. Kunao katika malipo ya karibuni walipata Sh36 na wengine wakapata Sh80. Ni wachache sana walipata Sh100. Vile washauri wa rais walifanya ni kuchukua ile bei ya juu katika mnada na kuitangaza kuwa malipo kwa wakulima,” akasena Bw Miriti.

Mnamo Februari 3, Waziri wa Kilimo Peter Munya alikutana na wakulima wa zao hilo katika uwanja wa Ihura ulioko Kaunti ya Murang’a na akawaambia kuwa anaelewa kuwa kuna shida ya malipo duni katika sekta hiyo.

Alisema kwamba kuna hujuma kutoka kwa madalali, wasimamizi wa mashirika ya wakulima na pia wakora ili kuwanyima wakulima nafuu katika malipo.

“Hata wabunge wenu mnafaa muwaulize ni kwa nini huwa wanapinga miswada ya kubadilisha sera za malipo na hiyo ndiyo sababu kuu mnachukia serikali na rais wetu kufuatia malipo duni. Nawahakikishia kuwa tutarekebisha hali hiyo kupitia sera na mageuzi katika mashirika,” akasema kabla ya Rais kutangaza mnamo Februari 3 akiwa Ikulu ndogo ya Sagana kwamba bei imeimarika.

Hali ni iyo hiyo kwa wafugaji ambao wanalalamika kufuatia mfumko wa bei za chakula na madawa kwa mifugo, wakulima wakilia kupanda kwa bei ya fatalaiza ambayo pia imepunguka ubora na madalali kudidimiza bei za parachichi na mandizi nao wazalishaji maziwa wakiteta kukosa uthibiti wa bei hasa katika misimu ya mvua.

Katika mkutano wa Murang’a, Bw Munya alililiwa na wakulima aagize vitengo vya kiusalama viwakinge kutokana na wezi wa mazao ya kilimo ambao huyachuuza kwa madalali barabarani.

“Wezi wanaingia kwa mashamba yetu na kuvuna kahawa, majanichai, mandizi na maparachichi na kisha kufungua soko haramu la uchuuzi tukishuhudia,” akasema mkulima Rufus Njuguna.

Bw Munya alitangaza kuwa usalama wa mazao ya kilimo unafaa uzingatiwe na makamishna wa Kaunti, akimwelekeza wa Murang’a Bw Karuku Ngumo awajibikie kilio hicho cha Bw Njuguna.

Mkurugenzi wa Shirika la Utafiti wa masuala ya Kiuchumi la NewTimes Bw Wanjumbi Mwangi alisema kuwa “kutoa takwimu zisizo sahihi kuhusu maisha ya wananchi huangazia serikali kama inayodanganya kwa njia ya ukatili na hali huwa ni ya kuzidisha hasira kuihusu.”

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending