– Kakake Raila, Oburu Odinga alifuchua kuwa kiongozi huyo alikuwa amesafiri kwenda Dubai kwa ajili ya kupokea matibabu spesheli
– Raila alirejea nchini kimya kimya Jumapili Julai 12 na anaendelea kupata nafuu
– Gavana Joho na mbunge Junnet walimtembelea Raila akiwa hospitalini Dubai
Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga amerejea nchini kimya kimya majuma matatu baada ya kulazwa katika hospitali moja kule Dubai ambapo amekuwa akipokea matibabu.
Raila alitua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta Jumapili, Julai 12 akiwa ameabiri ndege yenye starehe yenye nambari ya usajili A318-112(CJ) Elite A6-CAS, MS4211.
Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, Raila alisafiri hadi nchini humo kufanyiwa upasuaji kwenye mgongo wake.
Gavana wa Mombasa Hassan Joho na mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed walimtembelea Raila hospitalini ambapo waliwajuza wananchi kuwa kiongozi wao alikuwa anaendelea kupata nafuu.
Gavana Joho na mbunge Junet Mohammed walimtembelea Raila hospitalini Dubai Source: Facebook
Wakenya mitandaoni walikuwa wamemtakia Raila afueni ya haraka pindi tu kakake Oburu Odinga alipofichua kuwa kiongozi huyo alikuwa ameondoka nchini kwa ajili ya matibabu spesheli.