Sinema ya bwerere ilizuka katika eneo la Kamunyolo huko kaunti ya Makueni baada ya mzee anayesemekana kuwa poifa ramli kumvamia lofa akimuonya dhidi ya kumtongoza binti yake.
Inaarifiwa kwamba buda aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kusikia uvumi mtaani kuwa barobaro huyo alikuwa na uhusiano wa mapenzi na msichana wake.
Kwa mujibu wa Taifa Leo, buda aliwaka akihisi jamaa amefanya kosa kubwa sana kwani mpango wake ulikuwa ni kumridhisha bintiye taaluma yake.
Alimkuta jamaa na kumzomea vikali na hata kumfuata kwake akimuonya akome kumtongoza msichana wake na kusambaratisha mipango aliyo nayo juu yake.
“Nimesema achana na msichana wangu. Koma hata kumpigia simu kabisa. Nikikuona naye tena walahi utakula nyasi. Hapo ndio utajua mimi ni mganga wa kweli,” mzee alifoka.
Penyenye zinasema baada ya jamaa kusikia mipango ambayo mzee alikuwa nayo kwa bintiye aliamua kukiri kosa lake na kuapa kwamba hatarudia kumnyemelea kipusa huyo tena.
“Nimekubali mzee. Hutawahi sikia tena nikimtomgoza binti yako. Wewe endelea na mipango yako ya kumridhisha kazi yako” jamaa alimueleza mzee huku waliokuwepo kushuhudia sokomoko hiyo wakipasua vicheko.
Mzee alimua kurudi nyumbani na kuahidi kumwadhibu vikali jamaa iwapo atasikia ameonekana tena na bintiye popote.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.