Jamaa aliyekodi nyumba ya kifahari ya mganga eneo la Kiritiri kaunti ya Embu alilazimika kuhama alipovamiwa na siafu baada ya kukataa kuoa bintiye mpiga ramli huyo.
Semasema za mtaani zinaarifu kuwa tangu lofa alipohamia katika nyumba hiyo, mpiga ramli huyo amekuwa akimshawishi amuoe msichana wake.
Siku ya kioja jamaa alifurushwa katika jumba hilo na siafu waaliomshambulia nyakati za usiku akiwa amelala.
Siku ilifuata lofa alisikika akinung’unika kwamba mpiga ramli huyo alipanga kulipiza kisasi baada yake kukataa kuwa na uhusiano wa mapenzi na bintiye na ndiposa akawatuma siafu kumkosesha usingizi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.