Connect with us

General News

Bei ya mahindi yatarajiwa kuzidi kupanda wasagaji wakidinda kuyaagiza kutoka nje – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Bei ya mahindi yatarajiwa kuzidi kupanda wasagaji wakidinda kuyaagiza kutoka nje – Taifa Leo

NJENJE: Bei ya mahindi yatarajiwa kuzidi kupanda wasagaji wakidinda kuyaagiza kutoka nje

NA WANDERI KAMAU

WASAGAJI mahindi nchini wamekataa kuagiza mahindi kutoka nje, kutokana na gharama kubwa ya usafirishaji na muda mfupi uliotolewa na serikali kuwaruhusu kusafirisha zao hilo kutoka mataifa ya nje.

Ni hali inayotajwa kuwa itachangia bei ya unga wa mahindi kuendelea kupanda.

Wasagaji wanasema kuwa kwa sasa, wanaweza tu kupata akiba nzuri ya mahindi hayo kutoka Mexico, ambapo itachukua angaa siku 45 kwa mahindi hayo kufika nchini.

Wiki iliyopita, serikali ilipunguza ushuru unaotozwa mahindi yanayoingizwa nchini kutoka mataifa yaliyo nje ya ukanda wa Afrika Mashariki kwa asilimia 50, ili kuwaruhusu wasagaji kuagiza mahindi zaidi kukabili bei ya juu ya unga iliyopo kwa sasa.

Serikali imewaruhusu kuingiza hadi tani 540,000 za mahindi.

“Tumekuwa na changamoto ambazo zinaifanya kuwa vigumu kwetu kuyaagiza mahindi hayo katika muda uliotolewa. Miezi mitatu ni muda mfupi sana kuagiza kiwango cha kutosha cha mahindi nchini,” akasema Bw Jajan Shah, ambaye ndiye Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Capwell Industries.

Bw Shah alisema kuwa bei za mahindi katika kiwango cha kimataifa ni za juu sana, hali inayowafanya wasagaji wengi kutozingatia kuyaagiza kutoka nje.

Mwenyekiti wa chama cha United Grain Millers Association—kinachodhibiti asilimia 80 ya sekta ya unga nchini, Bw Ken Nyagah, pia amesema kuwa uagizaji mahindi hautapunguza bei ya unga kutokana na gharama ya juu za uzalishaji.

“Gunia moja la mahindi yanayosafirishwa kutoka nje linauzwa kwa Sh6,000. Hata hivyo, kiwango hicho hicho cha mahindi kinauzwa Sh4, 700 nchini. Hilo linamaanisha kuwa mahindi yanayosafirishwa nchini kutoka nje hayatachangia lolote katika kupunguza bei ya unga,” akasema Bw Nyagah.

Mwenyekiti huyo pia alieleza hofu kuhusu hatua ya serikali kuwahusisha wasagaji kuyaingiza mahindi hayo nchini.

Alisema kuna uwezekano wa baadhi ya wafanyabiashara walaghai kuyaingiza mahindi hayo na kuyaficha.

Alisema wengi wao huyatoa baada ya bei za unga kupanda sana ili kujipatia faida kubwa.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending