[ad_1]
Benki yatwaa hoteli ya English Point Marina kufuatia deni la Sh5.2b
NA OTIATO GUGUYU
BENKI ya KCB imechukua usimamizi wa hoteli ya kifahari ya English Point Marina iliyo Kaunti ya Mombasa, baada ya kampuni ya Pearl Beach Hotels inayoimiliki, kushindwa kulipa deni la Sh5.2 bilioni.
Kampuni hiyo imekuwa ikitatizika kugharimia deni hilo kwa KCB katika miaka iliyopita. Duru zilifichua kuwa, KCB ilitwaa usimamizi wa kampuni na hoteli hiyo mnamo Jumanne na kuiweka chini ya usimamizi wa mrasimu.
Mrasimu atatarajiwa kuuza sehemu au jumba zima ili kupata fedha za kutosha kulipa deni ambalo KCB inadai.Hoteli hiyo humilikiwa na Bw Amin Kanji, mkewe Leila, kakake Alnoor, na jamaa zao.
Next article
Wimbi la uhalifu Pwani
[ad_2]
Source link