Akizungumza na Keziah Kariuki, mama huyo wa watoto wawili alifichua kuwa kuanzia mwanzo ndoa yake ilikuwa na mzuka ambao ulimfanya kupigana sana.
Kulingana naye, aliingia katika mahusiano na Kanyari baada ya mchumba wake wa wakati huo kumtema wiki tatu kabla ya kumtabulisha kwa familia yake.
“Nilikutana na Kanyari wakati nilikuwa nimekwenda kuimba katika kanisa lake. Alinialika baadaye na kunishukuru kwa kuwatumbuiza.Alikuwa katika uhusiano mbaya. Jamaa niliyekuwa namchumbia wakati huo alikuwa anatakiwa kuja kwetu kukutana na mama yangu lakini alikosa kuja. Nilikuwa nimeandaa kila kitu. Wakati nilikuwa nazungumza na Kanyari, nilimtania aje ajifanye kama mpenzi wangu na akakubali,” alisema. Bayo.
Baada ya kuanza kuishi pamoja na pasta huyo, Bayo alisema alitambua kuwa mume wake alikuwa anaishi na wafanyakazi wengine saba.
Kulingana naye,wafanyakazi hao hawakuwa na mipaka na wangeingia katika chumba chao cha kulala wakati wowote bila kubisha.
“Wakati nilihamia katika nyumba ya Kanyari, niligundua kuwa alikuwa anaishi na wanawake wengine sita.Wafanyakazi hao hawakuwa na mipaka na waliingia chumbani mwangu walivyotaka. Hawakuwa wakibisha. Sikuwa na faragha,” alisema Bayo.
Alifichua kuwa hakuwa na mamlaka yoyote ya kufanya maamuzi katika nyumba yake na wanawake hao ndio walikuwa wakimvisha mume wake.
“Wacha nikuambie hawa wanawake walikuwa wanaingia chumbani mwetu na kuchagua nguo ambazo mume wangu angevaa. Niliwapiga vita lakini nilichoka,” Bayo alisema.
Mama huyo msimbe alifichua kuwa wakati mwingine alilazimika kudanganya kanisani jambo ambalo alijua sio sawa.
“Sikuwa nafurahia kwenda kanisani. Nilikerwa kwa sababu alikuwa anadanganya kanisani. Siku moja alidanya kuwa nyumba yetu ilivamiwa na ilibidi nidanganye. Wakati moja pia alinilazimisha kukubali kuwa ameninunulia gari,” alisimulia msanii huyo.
Kulingana na msanii huyo, mama mkwe wake alikuwa anamlazimisha kumuunga Kanyari mkono ili kuhakikisha huduma hiyo inaendelea.
Mama yake Kanyari alikuwa akimpea Bayo mshahara wa KSh 30,000 kila Jumapili ili aweze kuandamana na Kanyari kanisani
“Mama yake alinepea ofa na kuniomba niwe nikienda kanisani kila Jumapili na mume wangu badala ya kurandaranda katika makanisa tofauti nikitafuta pesa. Alijitolea kunipa mshahara wa KSh 30,000 kila Jumapili lakini nilikataa. Alimuaru mwanawe asiwahi kunipa pesa zozote,” aliongezea mwimbaji huyo.
Awali, Beti alifichua kuwa wawili hao hawakuhalalisha ndoa yao kupitia harusi ya kanisani wala hata ya kitamaduni ama kuchukua hati ya kiapo.
Mama huyo msimbe ambaye aliondoka kwa uhusiano huo baada ya kuzuka kwa kashfa ya KSh 310, alifichua kwamba alianza kuishi pamoja na mtumishi huyo wa Mungu wiki tatu baada ya wao kuchumbiana.