[ad_1]
Chager achukua uongozi wa EA Safari Classic Rally siku ya pili
Na GEOFFREY ANENE
Mkenya Baldev Chager amechupa kileleni mwa mbio za magari za East African Safari Classic baada ya kutawala siku ya pili hapo Ijumaa.
Alinufaika pia na magari ya kiongozi wa siku ya kwanza Ken Block na bingwa mtetezi Rosenberger kukumbwa na matatizo.
Muingereza Block akishirikiana na Alessandro Gelsomino walikamilisha siku ya kwanza ya mashindano haya ya siku tisa mnamo Februari 10 katika nafasi ya kwanza katika maeneo ya Naivasha (Elementaita, Kipsaos na Kiptagich) wakiendesha gari la Porsche 911 SC Proto.
Chager, ambaye alikamata nafasi ya tatu katika siku ya kwanza nyuma ya Block na raia wa Austria Rosenberger/Niki Bleicher (Porsche 911 SC Proto), alisalia katika nafasi hiyo katika mkondo wa nne katika eneo la Aberdare nyuma ya Philip Kadoorie/Ryan Champion (Porsche 911) na Mkenya Piers Daykin/Pierre Arries (Datsun 240Z).
Alikwamilia nafasi hiyo eneo la Moguni nyuma ya Daykin na Mswidi Patrik Sandell/Henrik Bolinder (Porsche 911 Proto). Alirukia nafasi ya pili mkondo wa sita (Loldaiga) nyuma ya Block na mbele ya Mkenya Ian Duncan/Anthony Nielsen (Rover SD1 Vitesse) akinufaika na Sandell na Daykin kuteleza.
Baada ya siku mbili za kwanza za jumla ya kilomita 418.55, Chager aliongoza mbio hizo za kilomita 3,474.65 (kilomita 1,804 za kushindania pointi) kwa saa 5:04:58.8. Sandell (5:07:06.0), Block (5:08:56.2), Duncan (5:10:24.4) na Daykin (5:11:36.0) walikamilisha tano-bora. Juamosi, madereva wataelekea maeneo ya Il Polei (kilomita 116.50), Ewaso (kilomita 89.00) na Golf Gate (kilomita 54.53). Madereva 46 walianza mashindano yatakayopitia katika kaunti 11, lakini karibu 10 akiwemo Quinten Mitchell walikuwa wamejiuzulu kufikia Ijumaa.
Next article
Menengai na Strathmore kikaangoni Kenya Cup
[ad_2]
Source link