Connect with us

General News

Chombo chapiga jeki ukaushaji mazao – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Chombo chapiga jeki ukaushaji mazao – Taifa Leo

MITAMBO: Chombo chapiga jeki ukaushaji mazao

Na RICHARD MAOSI

KWA miaka mingi mazao yamekuwa yakikaushwa kwa kuanikwa juani.

Lakini kadri miaka inavyosonga, mbinu tofauti na teknolojia zimeendelea kuibuka kufanikisha ukaushaji wa mazao hasa mboga na matunda.

Mojawapo ya mbinu za kisasa ni utumizi wa chumba maalum kinachofahamika kama solar drier, ambapo matunda na mboga yanaweza kukaushwa kupitia nishati ya jua.

Mchakato wa ukaushaji mazao hutegemea mzunguko wa hewa na joto ndani ya chumba hicho cha solar drier.

Sawia na binadamu ambaye anahitaji hewa safi ya kuzungusha virutubishi mwilini, vilevile mimea inastahili kukaa katika mazingira ambayo ni safi na ya asilia dhidi ya wadudu wala vimelea vya fangasi na bakteria.

Imebainika kuwa asilimia 40 ya mazao hupotea kwa sababu ya ukosefu wa mbinu sahihi ya kuyahifadhi, jambo ambalo husababisha hasara kwa wakulima wadogo mashinani.

Hata hivyo, teknolojia inaonyesha kuwa mchakato wa kukausha mazao unaweza kufanyika kwa njia rahisi kupitia aina maalum ya chombo cha kupitisha hewa safi.

Ni mtambo ambao hutumika kufanikisha mzunguko wa hewa na joto mara nyingi katika viwanda vya kuhifadhi na kusindika vyakula, kutunza ubora wa mazao na kupunguza uharibifu wa bidhaa za matunda na mboga.

“Gharama ya kuendesha chombo hiki ni nafuu kwani huendeshwa na upepo kinyume na aina nyingine ya chombo cha kupitisha hewa ambacho huendeshwa kwa mafuta ya diseli au umeme,” anasema Juliet Odhiambo kutoka eneo la Sega, Kaunti ya Siaya.

Anasema kiwango cha hewa inayoingia ndani ya solar drier ndio huharakisha muda ambao mazao huchukua kukauka, isitoshe ni kifaa ambacho kina uwezo wa kuboresha hewa. Mfumo huu safi wa kuleta hewa hushirikisha ventileta ambazo huwa zimewekwa juu ya solar drier na huzunguka kwa kutegemea upande ambao upepo unaelekea.

“Kwa kuwa uingizaji hewa unategemea msukumo ulioundwa ndani ya solar drier, ambayo kwa kawaida hutokana na tofauti ya joto pamoja na kasi ya upepo,” anasema.

Msukumo huu ndio hubadilisha usambazaji hewa, na uwezekano wa kutoa hewa ambayo huwa imechafuliwa.

Ventileta zimetumika zaidi katika viwanda , ili kupunguza joto lililokithiri kupita kiasi , pamoja na kutengeneza mazingira safi ya kufanyia kazi

Hii ndio maana mnamo mwaka wa 2020, Juliet alianzisha mradi wa kukausha mihogo, akiwa na lengo la kutafutia soko wakulima wadogo bidhaa zao.

Pili, alitaka kuimarisha bei ya bidhaa zao kwa kuongezea mihogo thamani ambayo hatimaye huuzwa kama unga wa kuandaa vitafunio kama maandazi , chapati na keki, katika masoko ya nje jijini Nairobi.

Juliet ambaye anamiliki solar drier mbili anaungama kuwa kwa wiki moja anaweza kununua kilo 1,200 za mihogo ambazo huchukua muda wa kati ya saa 24-48 kukauka.

Kwa upande mwingine, Erick Owino ambaye ni mtaalam wa kukausha mazao anasema mradi kuna mzunguko wa hewa safi ndani ya chumba cha kukausha mazao, bila shaka mkulima atapata manufaa mengi, mojawapo ikiwa ni kuhakikisha kuwa yanadumisha ubora.

Mtaalam wa kukausha mazao ya kusindika Bw Erick Owino akionyesha aina maalum ya mtambo wa vipumuzi almaarufu kama ventilators ambavyo husaidia kuimarisha mzunguko wa hewa safi ndani ya solar drier. PICHA | RICHARD MAOSI

Aidha huzuia uwezekano wa vimelea vya bakteria kukua juu ya mazao, jambo ambalo huonyesha kuwa mfanyibiashara anaendesha kilimo biashara chenye tija.

Pia anaeleza kuwa ventileta hizo hutumika kama vichungi kuchuja uchafu usifikie sehemu ya kuhifadhia mazao ya shambani.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending