[ad_1]
DCI wachunguza bunduki iliyoua mtoto wa mbunge
NA ROBERT KIPLAGAT
WAPELELEZI katika Kaunti ya Narok wanachunguza bunduki iliyotumiwa na mwanawe Mbunge Maalum, David ole Sankok kujitoa uhai Jumatatu.
Akizungumza na wanahabari katika afisi yake, Mkurugenzi wa DCI katika Kaunti ya Narok, Mwenda Ethaiba, alisema bastola hiyo imepelekwa kufanyiwa uchunguzi katika makao makuu ya DCI jijini Nairobi.
Mwanawe Bw Sankok mwenye umri wa miaka 15 aliyetarajiwa kujiunga na Kidato cha Tatu katika Shule ya Upili ya Kericho, anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi ndani ya chumba chake katika eneo la Ewaso Ng’iro, Kaunti ya Narok.
Bw Ethaiba alisema wapelelezi watachunguza jinsi bunduki hiyo ilivyopatikana, iwapo ina leseni au inamilikiwa kwa njia isiyo halali.
Mwili wa mvulana huo ulifanyiwa upasuaji Jumanne jioni na mtaalamu wa serikali katika Hospitali ya Wilaya ya Longisa katika kaunti jirani ya Bomet.
“Uchunguzi wa ripoti ya upasuaji ulithibitisha kuwa kifo cha mwendazake kilisababishwa na risasi iliyopitia kwenye kidevu cha mtoto huyo na kutokea kichwani mwake,” alisema Bw Ethaiba.
Alisema wapelelezi walirekodi taarifa kutoka kwa watu 10 akiwemo mbunge huyo na mkewe Hellen, binti yao mkubwa pamoja na wafanyakazi katika hoteli ya mwanasiasa huyo ya Osim Country Lodge iliyo kwenye boma la familia hiyo.
Wapelelezi vilevile wanachunguza jinsi mtoto huyo alivyofikia silaha hiyo iliyosemekana kuhifadhiwa katika chumba cha baba yake.
Awali, mvulana huyo alikuwa amekataa kurudi shule.
Baada ya mazungumzo ya kina na baba na dada yake, alikubali kwenda lakini akajiua kwa kujipiga risasi dakika kadhaa baadaye.
Next article
NGUVU ZA HOJA: Matunda ya kwanza kabisa ya mtaala mpya wa…
[ad_2]
Source link