Akina mama wakiuza bidhaa zao sokoni. Picha: UGC Source: UGC
Kwa mujibu wa Taifa Leo, lofa alifika katika kibanda cha mama na kuagiza sukuma wiki za shilingi hamsini lakini baada ya mama kumkatia mboga hizo alichomoa KSh 30 pekee.
Mama alipojaribu kumuuliza jamaa kuhusu salio la KSh 20, lofa alimwambia angeleta siku inayofuata.
Hata hivyo, mama mboga aliwaka akimlaumu jamaa kwa kuwa mgumu wa kulipa madeni huku akiwataja akina mama wengine wa vibanda ambao wamemlalamika.
Alimrukia barobaro na kumzaba kofi moja ya kishua ambapo lofa alijikuta yuko chini bila shati.
“Mtandike kabisa. Usimpe shati lake,” mama mboga mmoja alisikika akisema.
Duru zinaarifu kuwa jamaa alijaribu kuomba msamaha lakini wapi!
“Ukora wako leo utaisha! Utaneda kwako ukiwa uchi. Ujue pia sisi hizi mboaga sio hati tunakopeshwa,” mama alimfokea jamaa huku akimwachilia kwenda zake bila shati.
Inasemekana kila mmoja liabki amekodoa macho kuona sinema ya bure pasi na kumuokoa jamaa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.