Connect with us

General News

Dereva ashtakiwa kwa kutusi polisi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Dereva ashtakiwa kwa kutusi polisi – Taifa Leo

Dereva ashtakiwa kwa kutusi polisi

NA RICHARD MUNGUTI

DEREVA wa matatu mwenye lugha chafu na tabia mbaya Alhamisi alishtakiwa kuzua vurugu kwa kumtukana afisa wa polisi mwanamke.

Samuel Mwangi Githinji amekana mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Nairobi Bi Wendy Kagendo kwamba alimtukana afisa wa polisi mwanamke katika steji ya Ambassadeur, Nairobi.

Githinji aliye na umri wa miaka 30 alikabiliwa na shtaka la kuwa na tabia mbaya kinyume cha sheria nambari 94 (1) za uhalifu.

Alidaiwa mnamo Mei 29, 2022 kwenye barabara ya Moi Avenue alionyesha utundu kwa kumtukana afisa wa polisi mwenye cheo cha Koplo.

Bi Kagendo alielezwa Githinji alimkaripia Koplo Virginia Karimi akisema,“Wewe usiniletee umalaya hapa.”

Kiongozi wa mashtaka Bi Nancy Kerubo amesema kwamba matamshi hayo ya Githinji yalilenga kumuudhi Koplo Karimi.

“Sipingi mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana,” Bi Kerubo ameeleza mahakama.

Bi Kagendo alimwuliza mshtakiwa ikiwa aliachiliwa kwa dhamana na polisi alipokamatwa.

“Uliachiliwa kwa dhamana na polisi ulipokamatwa?” Bi Kagendo amemwuliza mshtakiwa.

“Ndio. Niliachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu Sh20,000,” mshtakiwa amejibu.

Hakimu amemwachilia mshtakiwa kwa dhamana kiasi sawa na hicho alichokuwa amepewa na msimamizi wa kituo cha polisi cha Central.

Kesi itatajwa Juni 16, 2022 kwa maagizo zaidi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending