[ad_1]
Dereva Kimathi kupata mafunzo ya Equator Rally kutoka kwa nyota Tapio
Na GEOFFREY ANENE
Bingwa wa Afrika mbio za chipukizi McRae Kimathi atapata mafunzo tena kuwa kwa kutoka kwa dereva mtajika Tapio Laukkanen kabla ya duru ya pili ya Mbio za Magari za Afrika (ARC) Equator Rally itakayofanyika Aprili 1-3.
Kimathi, 27, ameanza Machi 5 matayrisho ya Equator Rally siku chache baada ya kupokelewa kwa shangwe na maafisa wa Mbio za Magari Duniani (WRC) na Kenya Airways kutoka Uswidi mnamo Machi 2.
Anafanyia majaribio gari lake la Ford Fiesta R3 kama sehemu ya maandalizi haya. “Nitapata mafunzo kutoka kwa Tapio Laukkanen kutoka Finland. Namtarajia nchini mnamo Machi 27,” alisema Mwafrika huyo wa kwanza kabisa kukamilisha Rally Sweden mnamo Februari 24-27.
Kabla ya mashindano ya Uswidi, Kimathi pia alikuwa amepokea mafunzo kutoka kwa maafisa mbalimbali wa fani hiyo akiwemo bingwa wa Mbio za Magari za Kitaifa za Kenya (KNRC) mwaka 2016 Laukkanen. Kimathi alimaliza Equator Rally nafasi ya nane mwaka 2020. Duru nyingine za WRC atakazoshiriki 2022 ni Croatia (Aprili 21-24), Ureno (Mei 19-22), Estonia (Julai 14-17), Safari Rally (Juni 23-26) na Ugiriki (Septemba 8-11).
Next article
Karan Patel mawindoni kumaliza nuksi Nakuru Rally
[ad_2]
Source link