– Walioshuhudia kisa hicho walisema gari hilo lilionekana likiendeshwa kwa kasi Jumamosi, Julai 4 kuelekea hospitalini huku taa zikiwa zimewashwa
– Wakazi walisema gari hilo lilipiga honi mara kadhaa kwenye lango hilo lakini mabawabu wa hospitalini waliupuuza wakidhani Maina alikuwa mlevi
– Alilala usiku kucha ndani ya gari hilo huku madirisha yote na milango ikiwa imefungwa
– Mkewe alisema marehemu alitoka nyumbani asubuhi akiwa buheri wa afya
Wakazi wa mtaa wa Juja, Kiambu waliachwa na mshtuko baada ya dereva wa teski kuoatikana akiwa amega dunia karibu na lango la Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT).
Kiini cha kifo chake kilichotokea Jumapili, Julai 5 hakikubainika lakini hata hivyo katika hali ya kuchukua tahadhari mwili wake ulibebwa na watalaam wanauohusika na masuala ya COVID-19.
Wakazi wa Juja, waliachwa na mshtuko baada ya dereva wa teski kupatikana akiwa amega dunia karibu na lango la (JKUAT). Picha: Kenya alerts. Source: Twitter
Daily Nation iliripoti kuwa dereva huyo wa teksi aliaga dunia nje ya kliniki baada ya kushinda hapo Jumamosi, Julai 4 uisku kutwa.
“Zoezi nzima lilizua hofu. Wengi walidhani aliaga dunia baada ya kuugua virusi vya corona,” Charles Chege, nduguye marehemu ambaye alihudumu katika teski alisema.
“Nilikuwa nikiendesha hilo gari kabla yake kulichukua. Wakati watu walipoliona walidhani ni mimi niko ndani. Nilianza kupokea simu na jumbe kuanzia saa kumi na mbili asubuhi lakini nilipuuza na nikaendelea kulala,” Chege aliongeza.
Ili kuchukua tahadhari mwili wake ulibebwa na watalaam wanaohusika na masuala ya COVID-19. Picha: Kenya Alerts. Source: Twitter
Hata hivyo baada ya kupokea simu, aliyempigia aliniarifu kuwa wakazi walikuwa wanavunja madirisha ya gari hilo.
Alisema Maina hakuwa mgonjwa, semi ambazo ziliungwa mkono na mkewe marehemu Esther Wangari.
Wangari alisema mumewe alikuwa buheri wa afya alipoondoka nyumbani asubuhi kwani hata hakuwa akipiga chafya.
Wenyeji walimpigia Charles Chege nduguye marehemu wakidhani kuwa ni yeye alikuwa ndani ya gari hilo. Picha: Daily Nation. Source: UGC
Alidokeza kuwa mdomo wake ulikuwa umekauka wakati alipatikana ameaga dunia.
Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, gari hilo lilionekana likiendeshwa kwa kasi huku taa zikiwa zikiwa zimewashwa kabla ya kupatikana likiwa limeegeswa Jumapili.
Wakazi walisema gari hilo lilisikika lipiga honi mara kadhaa majira ya saa nane mchana lakini mabawabu wa hospitalini walipuuza wakidhani Maina alikuwa mlevi.