Connect with us

General News

Diana B atakiwa afute kabisa mkanda – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Diana B atakiwa afute kabisa mkanda – Taifa Leo

KASHESHE: Diana B atakiwa afute kabisa mkanda

Na THOMAS MATIKO

MAHAKAMA imetishia kumchukulia hatua kali mke wa msanii Kevin Bahati, endapo hataifuta video aliyopakia YouTube, akidai Willy Paul aliwahi kujaribu kumbaka.

Baada ya kusikiliza upande wa malalamishi kwenye kesi hiyo iliyowasilishwa na Pozee, Hakimu Mkuu Mwandamizi D.W Mburu wa mahakama ya Milimani, Nairobi alitoa agizo kwa Diana kuifuta video hiyo mara moja.

“Baada ya kusikiliza upande wa malalamishi, mahakama inamwamrisha mshatakiwa kuifuta video chini ya kichwa ‘My Untold Story, Willy Paul Attempted to rape me’ kwenye akaunti yake ya YouTube na mitandao yake yote ya kijamii.

“Aidha posti zozote zenye madai hayo zinapaswa kufutwa kwa kuwa zinalenga kumchafulia jina mlalamishi na kumsababishia kupoteza fursa nyingi za kibiashara,” Hakimu Mburu kaamrisha.

Video hiyo iliyopakiwa mtandaoni wiki mbili zilizopita imefanikiwa kuvutia zaidi ya views laki nane kwenye YouTube kufikia kipindi uamuzi wa mahakama unatolewa.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending