– Wabunge wakosoaji wa DP Ruto wamefaidika na nafasi kwenye kamati za bunge
– Hilo lilifanyika baada ya wandani wa Ruto kutimuliwa kutoka nyadhifa zao na chama cha Jubilee
– Chama cha ODM ndicho kimeonekana kufaidika pakubwa na mzozo ndani ya Jubilee
Kundi la wabunge kutoka mrengo wa upinzani na ule wa Kieleweke ndani ya Jubilee lilizawadiwa baada ya wandani wa Naibu Rais William Ruto kutimuliwa kutoka nafasi kadhaa.
Aidha chama cha ODM ndicho kimeonekana kuvuna matunda zaidi kutokana na urafiki mpya wa kisiasa kati ya Raila Oduinga na Rais Uhuru Kenyatta.
Wandani wa DP Ruto bungeni walitimuliwa na nafasi zao kupewa wakosoaji wake. Picha: Citizen Source: Facebook
Wandani wa DP Ruto waliokuwa wakishikilia nyadhifa kama vile Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wah, Gladys Shollei wa Uasin Gishu, Moses Kuria wa Gatundu na wengine walitimuliwa kutoka nafasi walizokuwa wakishilia bungeni.
Wengine ni Alice Wahome wa Kandara, Wangui Ngirici wa Kirinyaga na William Cheptumo ambao walikuwa kwenye nafasi muhimu bungeni.
Ichung’wah alipoteza nafasi yake kama mwenyekiti wa kamati ya Bajeti kwa mbunge wa Kieni Kanini Kega.