Aden Duale kwenye picha ya awali. Duale ni mmoja wa wandani wa DP Ruto waliotimuliwa kutoka nyadhifa zao. Source: UGC
Wafuasi wote wa Ruto waliokuwa wakishikilia nyadhifa bungeni na kwenye seneti walitimuliwa na uongozi wa chama cha Jubilee.
Kwenye bunge la kitaifa, aliyekuwa kiongozi wa wengi Aden Duale pamoja na Kiranja Ben Washiali ni miongoni wa waliotimuliwa.
Aidha wabunge Gladys Shollei, Alice Wahome, Moses Kuria, Kimani Ichung’wa baadhi ya wengine walitimuliwa kutoka nafasi walizokuwa wakishikilia kwenye kamati mbali mbali.
Aliyekuwa naibu spika wa Seneti Kindiki Kithure. Kindiki alitimuliwa kutoka wadhifa wake kwa kuwa mwandani wa DP Ruto. Picha: Standard Source: Facebook
Aliyekuwa naibu spika wa Seneti Kindiki Kithure alitimuliwa kutoka wadhifa wake kwa kuwa mwandani wa DP Ruto.
Wengine walioangukiwa na shoka la Rais Uhuru Kenyatta ni aliyekuwa kiongozi wa wengi Kipchumba Murkomen na kiranja Susan Kihika.
Ni vita vilivyokuwa wazi kuwa vinawalenga wafuasi wa Ruto na siasa zake za urais 2022.
DP Ruto alisema wengi wanajipata pabaya kwa kuwa marafiki wake. Picha: DP Ruto Source: Facebook
Ruto, licha ya kuwa kimya walipokuwa wakitimuliwa, hivi maajuzi ameanza kuguruma na kusema wanahangaishwa kwa kuwa marafiki wake.
“Saa muombee hawa viongozi kwa sababu wengi wanahangaishwa, wanaambiwa watatumiwa KRA sijui EACC na makosa ni eti wao ni marafiki wa naibu rais wa Kenya,” alisema DP.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.