Connect with us

General News

Duale sasa amkejeli Rais – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Duale sasa amkejeli Rais – Taifa Leo

Duale sasa amkejeli Rais

NA GATUNI WACHIRA

Mbunge wa Garissa mjini Aden Duale ameilaumu serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kwa kile anachodai ni usaliti mkubwa ndani ya serikali.

Bw Duale jana alisema kwamba serikali ilikosa uwajibikaji katika kulinda katiba ambayo kulingana naye ndiyo imemwezesha Naibu wa Rais William Ruto kusimama jadidi kutetea maslahi ya Wakenya.

“Nataka nimwambie Rais Uhuru Kenyatta kwamba umefika wakati wa kutupilia mbali siasa za migawanyiko, siasa za uadui, siasa za udanganyifu na usaliti,” alisema Bw Duale.

Mbunge huyo ambaye hapo awali alikuwa kiongozi wa wengi katika Bunge la Taifa alisema kwamba Rais Kenyatta amekuwa akiongoza taifa hili kwa misingi ya migawanyiko, jambo ambalo limesababisha Wakenya wengi kuteseka.

Akiongea katika Uwanja wa Michezo wa Kimataifa wa Kasarani ambapo mkutano wa viongozi wa chama cha UDA ulikuwa umeandaliwa, Bw Duale alisema kwamba serikali ya William Ruto itahakikishia Wakenya usawa katika kila kitu.

Akimpongeza Naibu Rais kwa kuteuliwa kwake kuwania urais kwa tiketi ya chama cha UDA, mbunge huyo alisema kwamba uchaguzi ujao utakuwa kati ya maskini na matajiri.

“Nakupongeza sana Naibu wa Rais kwa kuteuliwa kuwania urais, lakini niseme kwamba uchaguzi ujao utakuwa kati ya matajiri na maskini,” alisema Duale.

Akionekana kurejelea awamu zilizopita, Bw Duale pia alisema kwamba wakati umefika taifa kuondokea uongozi wenye misingi ya familia na kuruhusu watu wengine kuliongoza.

Alisema kwamba awamu zilizopita zitazikwa kwenye kaburi la sahau,k wani Naibu Rais William Ruto atahakikisha kwamba historia ya kuwatesa manaibu wa marais haitajirudia.

“Uchaguzi ujao utahusu mabadiliko kabambe. Kwamba ili uwe kiongozi, lazima baba yako alikuwa kiongozi hapo zamani. Uongozi wa kifamilia tutauondoa kabisa na tutahakikisha kwamba kila Mkenya amesimamiwa vizuri. Naibu wa Rais mwenyewe amedhulumiwa,” alisema Duale.

Mbunge huyo mwenye tajriba pana katika siasa kadhalika amewasifu watunzi wa katiba ya Kenya ya mwaka 2010 kwa kazi ambayo kulingana naye ni mufti kwa vile imefafanua jukumu na kazi zote za Naibu wa Rais,pamoja na mchakato wote wa kumlinda.

“Nataka niwashukuru waliotungaa katiba yetu ya 2010. Wameandika vizuri kazi za naibu wa rais na ndicho kitu ambacho kimemfikisha Naibu wa Rais mpaka hapa tulipo. Bila shaka pasingekuwepo na vipengele vinavyomlinda Naibu wa Rais hatungefika hapa,” akadai Duale.

Bw Duale ambaye amekuwa mstari wa mbele kupinga mauaji yanayotekelezwa mara kwa mara,akisema kwamba mauaji haya yatazimwa katika serikali ijayo. Duale amesema kwamba wakenya wengi wameteseka kimawazo na kifikra,wanapozipata maiti za wapendwa wao kwenye mito.

“Wengi wa kina mama zetu wamewapoteza ndugu zao,kaka zao,waume zao katika vitendo hivi vya kinyama. Vitendo kama hivi vitafika tamati katika serikali ijayo,” akaongeza Duale.

Duale hata hivyo alijitetea vikali dhidi ya tetesi kwamba alivuliwa wadhifa wa Kinara wa wengi Bungeni,akisema kwamba tayari Rais Kenyatta alikuwa amempa heko kwa kufanya kazi vizuri,katika mkutano wao wa awali.

“Rais Kenyatta ni rafiki yangu wakiwa na Naibu wa Rais, lakini Rais alinihujumu kwa kukosa kumuunga mkono Naibu wa Rais,” alijisema Duale.

Katika mkutano alimokuwa akiongea huko Kasarani,zaidi ya washirika wa karibu wa Naibu wa Rais 5000 walihudhuria hafla hiyo,ambayo ilivutia maelfu ya wenyeji katika eneo hilo. Naibu wa rais ambaye alikuwa mgeni wa heshima naye alitoa ahadi tele kwa Wakenya,ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika fedha za humu nchini badala ya kukopa.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending