[ad_1]
Engesha kujiunga na Incheon Hyundai Steel Red Angels FC kutoka Vihiga Queens
Na GEOFFREY ANENE
Mshambulizi wa Vihiga Queens, Teresa Engesha Obunyu maarufu kama Terry yumo mbioni kujiunga na Incheon Hyundai Steel Red Angels nchini Korea Kusini.
Waajiri wake kutoka kaunti ya Vihiga wametangaza habari hizo Machi 19 wakisema kuwa wamefikia makubaliano na klabu hiyo ya Korea Kusini.
“Kamati Kuu ya Vihiga Queens inafurahia kutangaza kuwa Vihiga Queens imefikia mapatano na Incheon Hyundai Steel Red Angels nchini Korea Kusini kuhusu uhamisho wa mshambulizi hodari Tereza Engesha Obunyu maarufu kama Terry. Terry anatarajiwa kuelekea nchini Korea Kusini kujiunga na klabu hiyo mara tu atakapopata stakabadhi za kusafiri,” taarifa kutoka Vihiga Queens ilisema Jumamosi.
Klabu ya kinadada ya Incheon Hyundai Steel Red Angels ilianzishwa mwaka 1993. Inashiriki Ligi Kuu ya Korea Kusini.
Incheon Hyundai Steel Red Angels imeshinda ligi hiyo mara tisa mfululizo tangu 2013.
Engesha, ambaye ni mmoja wa wachezaji tegemeo katika timu ya taifa ya Harambee Starlets, atakuwa raia wa pili wa kigeni katika kikosi hicho baada ya mshambulizi Mbrazil Nenem.
Tangu Januari 2022, mabingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) Vihiga Queens wamepoteza wachezaji Lilian Awuor (kipa), Jentrix Shikangwa (mshambulizi), Christine Nafula (kiungo mshambulizi) na Engesha (mshambulizi). Awuor na Shikangwa walijiunga na Soyaux-Charente nchini Ufaransa na Fatih Karagumruk nchini Uturuki mwezi Januari. Nafula alielekea Kayserispor nchini Uturuki wiki moja iliyopita.
Next article
Mapenzi kwao basi!
[ad_2]
Source link