Connect with us

General News

Evariste Ndayishimiye aapishwa rasmi kuwa rais mpya wa Burundi

Published

on

– Ndayishimiye ameahidi kulinda katiba ya Kenya, kutoa haki kwa wote na kulinda mipaka ya taifa hilo

– Maelefu ya raia wa Burundi walikusanyika katika uwanja wa Ingoma kusherehekea uapisho wake

– Rais huyo ameapishwa majuma mawili baada ya kifo cha ghafla cha Rais Pierre Nkurunziza

Maelfu ya raia wa Burundi wamekusanyika katika uwanja wa Ingoma mkoani Gitega kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Evariste Ndayishimiye kama rais.

Sherehe hiyo ya uapisho inatokea majuma mawili baada ya kifo kwa rais Pierre Nkurunziza ambaye alikuwa aondoke mamlakani mwezi Agosti.

Evariste Ndayishimiye aapishwa kuwa rais mpya wa Burundi

Evariste Ndayishimiye sasa ndiye rais mpya wa Burundi

Viongozi kadhaa kutoka Barani Afrika akiwemo naibu rais wa Tanzania Samia Suluhu na aliyekuwa rais nchini humo Jakaya Kikwete wamehudhuria sherehe hiyo.

Ndayishimiye ameahidi kulinda katiba, kuheshimu umoja wa wananchi, kutoa haki kwa wote na kutetea mipaka ya taifa hilo.

Burundi ilifanya uchaguzi mkuu Mei 20 ambapo Rais mtarajiwa Ndayishimiye aliibuka mshindi.

Comments

comments

Facebook

Trending