Connect with us

General News

Familia yapinga bunge kujadili mzozo wa ardhi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Familia yapinga bunge kujadili mzozo wa ardhi – Taifa Leo

Familia yapinga bunge kujadili mzozo wa ardhi

NA BRIAN OCHARO

FAMILIA ya Saggaf inayomiliki ekari 289 za ardhi katika Kisiwa cha Wasini, Kaunti ya Kwale, inataka bunge la kitaifa lizuiwe kujadili umiliki wa ardhi hiyo.

Bw Mohamed Maula, ambaye amewasilisha kesi hiyo katika mahakama ya Mombasa kwa niaba ya familia hiyo, amesema hatua ya mbunge wa Lunga Lunga Khatib Mwashetani kuhusisha bunge la kitaifa katika suala hilo ina nia mbaya.

Kulingana naye, suala hilo lilihitimishwa na mahakama zaidi ya miaka 24 iliyopita walipopatikana kuwa wamiliki halali.

“Haki yetu ya kikatiba inatishiwa kubatilishwa na mchakato usio halali kwa kuingiliwa na bunge, na mahakama hii ina mamlaka ya kukomesha jaribio hilo,” alisema Bw Maula.

Ardhi hiyo ya thamani ya zaidi ya Sh2 bilioni imekuwa na mzozo kati ya familia hiyo na jamii za eneo hilo.