Connect with us

General News

Gavana Nyoro awarai wakulima wa Kiambu watie bidii kufukuza njaa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Gavana Nyoro awarai wakulima wa Kiambu watie bidii kufukuza njaa – Taifa Leo

Gavana Nyoro awarai wakulima wa Kiambu watie bidii kufukuza njaa

NA LAWRENCE ONGARO

WAKULIMA wapatao 2,000 kutoka eneo la Ngoliba, Thika Mashariki, wamepokea mbegu za mahindi na maharage ili kupanda kwenye mashamba yao.

Wakazi wa kijiji cha Magogoni, na maeneo mengine ya karibu walijitokeza kwa wingi kupokea mbegu hizo zilizotolewa na serikali ya kaunti ya Kiambu.

Gavana wa Kiambu Dkt James Nyoro, alizuru eneo hilo kujionea mwenyewe jinsi wakazi hao walivyopokea mbegu hizo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya upanzi.

Alitoa wito kwa wakazi hao kujiandaa mapema kuona ya kwamba wanapanda mbegu za mahindi na maharage hayo huku wakitarajia mvua kunyesha hivi karibuni.

“Ninatoa ushauri kwenyu mjiandae kuona ya kwamba mnakwenda kwenye mashamba yenu ili kupanda mbegu mlizopokea,” alifafanua Bw Nyoro.

Alisema kwa siku za hivi karibuni imekuwa wazi ya kwamba hali ya maisha inaendelea kupanda na kuwa ngumu maradufu.

Kwa hivyo aliwaambie wasilaze damu bali wafanye bidii kuona ya kwamba wanajitegemea kwa kulima mashamba yao wakingoja kuvuna jasho lao.

Alisema hivi karibuni wataalam wa kilimo watatumwa mashinani ili kuwahamasisha.

Gavana huyo pia aliwashauri wakazi hao kutouza mbegu hizo huku akisema kumekuwa na ukame katika sehemu nyingi nchini.

Bw Samuel Kimani ambaye ni mkazi wa kijiji cha Magogoni, alipongeza juhudi za gavana kuwajali wakazi wa eneo hilo kwa kutoa mbegu za mahindi na maharage.

Alieleza kuwa mwaka uliopita wa 2021, wakazi wengi walinufaika na msaada huo.

Alitoa mfano wake jinsi alivyonufaika pakubwa na msaada huo.

“Natoa mfano wangu kwa sababu mwaka 2021 nilipokea paketi mbili za mbegu za mahindi na baada ya kuzipanda nilipata magunia 10 ya mahindi,” alifafanua Bw Kimani.

Alitoa wito kwa wakazi hao wajitoe mhanga kuona ya kwamba mbegu hizo zinawanufaisha pakubwa.

Aliwashauri wakazi wa eneo hilo wasije wakapewa ahadi za uwongo na viongozi wanapotafuta vyeo vya uongozi.

Aliwashauri wajaribu kuwadadisi viongozi hao ambao “kwa wakati huu watakuja na ahadi nyingi zisizo na msingi.”

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending