Connect with us

General News

Gavana Twaha apuuzilia mbali EACC kuhusu ripoti ya ufisadi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Gavana Twaha apuuzilia mbali EACC kuhusu ripoti ya ufisadi – Taifa Leo

Gavana Twaha apuuzilia mbali EACC kuhusu ripoti ya ufisadi

NA KALUME KAZUNGU

GAVANA wa Lamu, Fahim Twaha amekanusha madai ya Tume ya Kupambana na Ufisadi nchini (EACC) kwamba alitumia vibaya ofisi yake kuajiri wafanyakazi isivyostahili.

Tume hiyo pia inapendekeza Katibu wa Serikali ya Kaunti ya Lamu, ambaye ndiye mkuu wa utumishi wa umma eneo hilo pia kushtakiwa kwa kuajiri wafanyakazi bila kuzingatia kuhitimu kwao kielimu.

EACC inaamini uajiri wa wafanyakazi wa kaunti ulitekelezwa bila kufuata mpangilio ufaao wa uajiri.

Katika ujumbe wake, aidha, Bw Twaha alieleza kutoridhishwa kwake na taarifa zinazoenezwa kwenye vyombo vya habari kwamba alikaidi sheria za uajiri wa wafanyakazi.

Bw Twaha alishikilia kuwa wafanyakazi wote wa serikali yake waliteuliwa na kuajiriwa kulingana na sharia.

Alishikilia kuwa wafanyakazi wanaodaiwa kuajiriwa isivyofaa ni wenye kuhitimu na wachapa kazi vizuri kiasi kwamba baadhi yao wametwaliwa na kuajiriwa na EACC yenyewe na pia Benki ya Dunia kutokana na weledi wao wa utendakazi.

Bw Twaha alisema maeneo ya kama vile Lamu ambayo yametelekezwa kwa muda mrefu hulazimu kuweka maafikiano ya kawaida na ya pamoja ya wanaoajiriwa katika harakati za kupiga vita dhuluma za kihistoria na kuleta amani na umoja.

“Kuajiri maafisa wachache kwa kandarasi fupifupi ili kujaza mapengo kila baada ya muda haimaanishi huo ni ukiukaji wa maadili au ufisadi. Hata hivyo tuko na haki ya kutafuta ushauri na ufafanuzi wa kikatiba kuhusiana na sheria za kusaidia kuamua iwapo madai ya uajiri mbaya uliofanyika kwa nia njema wafaa katika utawala wa ugatuzi,” akasema Bw Twaha.

Kaunti ya Lamu ina zaidi ya wafanyakazi 1000.Kauli ya Twaha ya kujitenga na madai ya EACC kuhusu ukiukaji wa sharia za uajiri inajiri muda mfupi baada ya gavana mwenzake wa Tana River, Dhadho Godhana pia amejitokeza kukanusha madai ya EACC kuhusu ufisadi.

Mbali na Bw Twaha na Bw Godhana, EACC pia inataka Gavana wa Kirinyaga, Anne Waiguru kushtakiwa na tayari imewasilisha faili kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Noordin Haji.

Gavana Waiguru amejipata matatani kuhusiana na madai ya kupokea Sh10 milioni kama marupurupu ya usafiri kwa safari ambazo katu hazikufanyika.

EACC inataka Gavana Waiguru na maafisa wengine wa serikali ya kaunti hiyo kushtakiwa kwa makosa ya kupanga na kutekeleza ufisadi na udanganyifu.