Connect with us

General News

‘Gooseberries’ ni matunda yaliyopuuzwa, wanayoyafahamu wanajua yana faida tele – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

‘Gooseberries’ ni matunda yaliyopuuzwa, wanayoyafahamu wanajua yana faida tele – Taifa Leo

‘Gooseberries’ ni matunda yaliyopuuzwa, wanayoyafahamu wanajua yana faida tele

NA SAMMY WAWERU

ENEO la Kwa Mbiu, mita chache kutoka barabara inayounganisha Ruaka, Tigoni na Limuru, Stephen Mwanzia ana furaha na tabasamu kutokana na kilimo-biashara alichokumbatia.

Ni mkulima hodari na mtaalamu wa matunda aina ya bukini, maarufu kama gooseberries pia golden berries.

Aidha, ni matunda yenye dhana kuwa yanakua msituni au kwenye vichaka, ila kwa Mwanzia ni dhahabu.

Allianza kilimo cha bukini, baada ya kuhudumu kama mtaalamu-mshauri wa masuala ya matunda mataifa kadha wa kadha Barani Afrika.

Na huu ukiwa mwaka wake wa nane katika ukuzaji wa bukini, Mwanzia anasema alijifunza mengi kuhusu matunda haya ya thamani nchini Rwanda.

Alifungua jamvi, kwa ekari 5 na kufikia sasa anastawisha kilimo cha matunda haya katika shamba la ukubwa wa ekari 20.

Kulingana na Mwanzia, bukini ni kati ya matunda rahisi mno kukuza, na yasiyohitaji mwalimu.

Huku suala la matumizi ya dawa na fatailaza zenye kemikali likizua mdahalo kuwa ni mojawapo ya visababishi vikuu vya maradhi kama vile saratani, mkulima huyu huzalisha matunda yake bila kutumia dawa zozote zile.

Huyapanda kwa kutumia mbolea ya mifugo, akisisitiza kwamba amekumbatia mfumo wa kilimohai (organic-farming), suala ambalo linafanya mazao yake kuwa mithili ya mahamri sokoni. Ili kukabili wadudu na magonjwa shambani, Mwanzia hupanda mahindi asilia, ya rangi nyekundu na manjano.

Safari yake hata hivyo katika kilimo cha matunda haya yenye tija chungu nzima kiafya haijakuwa rahisi. Ikizingatiwa kuwa ni matunda yanayoaminika kukua msituni, Mwanzia anaelezea kwamba safari ya kuhamasisha walaji umuhimu wa matunda haya kiafya, ili kupata soko haikuwa mteremko.

Matunda aina ya bukini yanakomaa miezi sita baada ya upanzi, na shughuli za mavuno zinatekelezwa kwa mikono, ambapo ameajiri wafanyakazi kadhaa…

Baada ya mavuno, shughuli inayofuata ni ya kuondoa maganda, kuchagua kwa mujibu wa hadhi na kuyapakia.

Mbali na bukini za manjano, Mwanzia pia hulima bukini nyekundu, nyeusi, kati ya nyinginezo.

Chini ya utambulisho wake, Stephen’s Natural Foods, mjasirimali huyu pia huongeza mazao yake thamani kwa kuunda juisi, mvinyo, na ‘jam’.

Ana ujumbe maalum kwa vijana kuhusu sekta ya kilimo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending