Huku wakijaribu kujisitiri bila mfadhili, klabu hicho kimekuwa kikiwategemea mashabiki wake kupitia wakfu wa Augmentin Fund.
Hata hivyo, hatua hiyo haijapunguza mzigo huo huku kocha wa klabu hiyo Steven Polack akifichua kwamba amelazimika kuanza kutumia akiba yake kujikimu.
“Kile natumia kununua chakula na kutimiza mahitaji ya familia yangu ni pesa ambazo nilianza kuweka akiba nikiwa na miaka 35. Mambo ni magumu sasa na wajua hatujakuwa tukipokea mishahara yetu kwa sababu ya kukosa ufadhili,” Polack aliambiaNairobi News.
Polack ni miongoni mwa wale waliathiriwa katika klabu hicho. Picha: Carol Radull. Source: Twitter
Kulingana na kocha huyo Muingereza, angekuwa anataabika endapo asingelikuwa ameweka akiba kutoka kwa taaluma yake ya ukufunzi.
“Sio kila mtu huweka akiba kwa sababu wakati mwingine kile wanapata wanatumia katika mahitaji yao lakini wacha tujaribu kutenga kitu kidogo. Ninataabika lakini mambo yangekuwa mabaya zaidi endapo singelikuwa na akiba,” aliongezea kocha huyo.
Polack aliteuliwa kocha wa K’Ogalo mnamo Agosti 2019, na kumrithi Hassan Oktay ambaye alijiuzulu.
Kocha huyo mwenye miaka 59, alikuwa kwenye harakati ya kuongoza mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Kenya kutwaa taji lao la 19 kabla ya kutangazwa mabingwa katika hali tatanishi.