Connect with us

General News

Guinea-Bissau wapoteza penalti na kuambulia sare tasa dhidi ya Sudan – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Guinea-Bissau wapoteza penalti na kuambulia sare tasa dhidi ya Sudan – Taifa Leo

AFCON: Guinea-Bissau wapoteza penalti na kuambulia sare tasa dhidi ya Sudan

Na MASHIRIKA

GUINEA-BISSAU walipoteza penalti muhimu katika mchuano wa Kundi D uliowakutanisha na Sudan kwenye fainali za Kombe la Afrika (AFCON) zinazoendelea nchini Cameroon.

Mkwaju huo uliochanjwa na Pele Judilson Mamadu katika dakika ya 82 ulipanguliwa na kipa Ali Abou Achrine huku Piqueti Brito Silva akishuhudia mpira aliorejesha langoni baada ya kutemwa na Abou ukigonga mwamba wa goli la Sudan.

Penalti hiyo ilitokana na tukio la Abou kumchezea visivyo Steve Ambri ndani ya kijisanduku.

Joseph Mendes wa Guinea-Bissau pia alishuhudia fataki yake ikibusu mhimili wa lango la Sudan katika kipindi cha pili kabla ya juhudi za Frederic Mendy kuzimwa na kipa Abou.

Awali katika Kundi D, Kelechi Iheanacho alikuwa amefungia Nigeria bao la pekee na la ushindi dhidi ya Misri ambao ni wafalme mara saba wa taji la AFCON.

Guinea-Bissau sasa hawajafunga bao katika kila mojawapo ya mechi tano zilizopita za AFCON na kwa sasa wana kibarua kigumu cha kutinga hatua ya 16-bora ya kipute hicho. Misri na mabingwa mara tatu Nigeria ndio wanaopigiwa upatu wa kusonga mbele kwa hatua ya muondoano kutoka Kundi D.

Sudan waliotawazwa mabingwa wa AFCON mnamo 1970, wananogesha kivumbi hicho mwaka huu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10 na walionekana kuridhika na alama moja chini ya kocha mshikilizi Burhan Tia.

Sudan walimpiga kalamu mkufunzi Hubert Velud mnamo Disemba 2021 baada ya kikosi chake kutong’aa kwenye kipute cha Arab Cup kilichoshuhudia waajiri wake wakifungwa mabao 10 bila kutikisa nyavu za wapinzani katika mchuano wowote kati ya mitatu.

Jaribio la pekee la Sudan langoni mwa Guinea-Bissau lilitokana na juhudi za Mohamed Abdelrahman mwishoni mwa kipindi cha kwanza japo kombora lake likadhibitiwa vilivyo na kipa Maurice Gomis.

Sudan sasa watavaana na Nigeria katika mchuano ujao wa Kundi D mnamo Januari 15, 2022 huku Guinea-Bissau wakionana na Misri siku hiyo.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending