Connect with us

General News

Hakuna kupimwa wazimu kwa washukiwa wa mauaji – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Hakuna kupimwa wazimu kwa washukiwa wa mauaji – Taifa Leo

Hakuna kupimwa wazimu kwa washukiwa wa mauaji

Na RICHARD MUNGUTI

WASHUKIWA katika kesi za mauaji hawatahitjika tena kupimwa utimamu wa akili zao kabla ya kusomewa mashtaka mahakamani.

Hii inafuatia uamuzi wa kihistoria wa mahakama kuu Ijumaa wiki iliyopita. Katika uamuzi huo , Jaji Grace Nzioka alisema kupimwa akili kwa washukiwa wa mauaji kwapasa kuwa hiari na wala sio kushurutishwa.

Alisema kushurutisha kupimwa akili kwa washukiwa ni kukandamiza haki zao. Jaji Nzioka alisema hakuna sheria inayoamuru washukiwa wa mauaji wapimwe utimamu wa akili zao “kabla ya kushtakiwa.”

“Hakuna sheria inayoagiza washukiwa wapimwe akili kabla ya kujibu shtaka la mauaji,”alisema Jaji Nzioka. Jaji Nzioka alisema washukiwa wa mauaji wanapasa kupewa fursa ya kuamua ikiwa wangelitaka kupimwa utimamu wa akili zao au la.

Jaji huyo alisema kushurutisha mshukiwa wa mauaji kupimwa akili ni “kukaidi haki zake.” Uamuzi huo ulitolewa katika kesi ambapo afisa wa Polisi Msuya Ngolo Lewis alikataa kupimwa ikiwa akili yake ni timamu.

Wakili Danstan Omari anayemwakilisha Ngolo…Picha/RICHARD MUNGUTI

Akinukuu Kifungu nambari 25 cha Katiba, Jaji Nzioka alisema wananchi hawapasi kukandamizwa kwa njia yoyote ile. Jaji Nzioka alikubaliana na wakili Danstan Omari anayemtetea Lewis kwamba “kushurutishwa kupimwa utimamu wa akili kwa mshukiwa wa mauaji ni kukandamiza haki zake kwa mujibu wa Kifungu nambari 25 cha Katiba.”

Lewis ameshtakiwa kwamba alimuua Muktar Said Ibrahim katika eneo la Kona- Mbaya mtaani Mathare ulioko kaunti ndogo ya Starehe, Nairobi mnamo Novemba 12,2017. Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma alikuwa amewasilisha ombi Lewis azuiliwe rumande siku 10 ili apelekwe kupimwa akili.

“Mshtakiwa alikataa kupimwa akili ibainike ikiwa iko timamu au la,”Jaji Nzioka alifahamishwa na kiongozi wa mashtaka Bi Wangui Gichuhi. Bi Gichuhi aliomba mahakama iamuru afisa apimwe akili lakini ombi hilo likapingwa vikali na Bw Omari.

Kabla ya kusomewa shtaka ili ajibu, Lewis aliwasilisha tena ombi akipinga akishtakiwa. Kupitia kwa Bw Omari na mawakili Martina Swiga na Omaiyo Aranga aliomba mahakama ifutilie mbali kesi hiyo akidai mashahidi walioandikisha taarifa walielekezwa vile watakavyosema.

Bw Omari amesema Kifungu nambari 11 cha sheria za ushahidi, kinasema mashahidi katika kesi yoyote ile hawapasi kuelekezwa jinsi watakavyosema kortini mbali wanatakiwa kusema walichoshuhudia kwa hiari.

“Mashahidi katika kesi hii ni watu wa familia ya marehemu na walielekezwa jinsi ya kuandika taarifa za ushahidi na maafisa wa mamlaka huru ya polisi (IPOA),” Bw Omari alisema. Lakini kiongozi wa mashtaka Bw Solomon Waulikha na IPOA walipinga ombi hilo.

Bw Waulikha aliomba siku 14 kujibu ombi hilo la kuzimwa kwa shtaka hilo. Jaji aliamuru Bw Naulikha na IPOA wawasilishe tetezi zao kufikia Novemba 12,2021.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending