Akizungumza Jumatano, Juni 24 akiwa mjini Kilifi, Magoha alisema walimu watatakiwa kufika shuleni wiki mbili kabla ya shule kufunguliwa rasmi ili wapange ratiba ya jinsi masomo yatakavyoendeshwa.
Waziri huyo pia alisema kila mwanafunzi atapewa maski mbili na atakakiwa kuzingatia sheria ya kutokaribiana.
“Shule zote pia zitapewa vifaa vya kupima joto mwilini kwa kila mwanafunzi,” Alisema Magoha.
Haya yanajiri siku moja baada ya Magoha kutangaza kuwa kampuni ya Rivatex imepewa kibarua cha kushona zaidi ya maski 22 milioni zitakazosambazwa katika shule zote nchini.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.