[ad_1]
MALEZI KIDIJITALI: Hofu kuhusu usalama ipo ila usinyime kabisa mtoto vifaabebe
BAADHI ya wazazi wameamua kuwanyima kabisa watoto wao vifaabebe ili kuwaepusha na athari za mtandao.
Wataalamu nao wanapendekeza wazazi wasiwaruhusu watoto kudumu kwa mtandao kwa zaidi ya saa mbili. Hii ni kwa wale walio na umri wa zaidi ya miaka sita.
Vifabebe ni marufuku katika taasisi za masomo ya msingi. Hata hivyo, wanasaikolojia wanasema japo ni muhimu kudhibiti matumizi ya vifabebe miongoni mwa watoto, wazazi wanafaa kufahamu kwamba kila mtoto ni tofauti kutoka kwa mwingine.
“Usifananishe watoto. Kila mmoja ni tofauti na mwingine na hulka za watoto huwa ni tofauti sawa na mtizamo wao kuhusu mambo. Muhimu ni kuwasikiliza ili uelewe jinsi ya kuwashughulikia hasa kuhusiano na matumizi ya vifabebe na mtandao,” yanaeleza makala ya wataalamu wa malezi yaliyochapishwa kwenye jarida la Psychology Today.
Wanasaikolojia wanasema kwamba kwa kuwa mzazi hawezi kumsimamia mtoto wake kwa saa 24 ili aweze kuthibiti matumizi ya mtandao, anachofaa kufanya ni kusikiliza kila mmoja aelewe mtazamo wake kuhusu intaneti.
“Ndio sababu inapendekezwa mzazi asipatie mtoto blackout kuhusiana na masuala ya mtandao. Anachopaswa kufanya ni kupima mtazamo na uwezo wa kila mtoto bila kumfananisha na mwingine. Kwa kufanya hivi, mzazi huwa anawasaidia watoto wake kuthamini mtandao na teknolojia kwa jumla,” asema mtaalamu wa malezi John Kaveni.
Wanasaikolojia wanasema baadhi ya hatua ambazo wazazi wanachukua kudhibiti matumizi ya mtandao ya wanao zinaweza kufanya watoto kuuchukia na kudhani hauna faida katika maisha yao.
Wanasema wazazi wanafaa kusawazisha usalama wa watoto katika intaneti na maslahi yao ya siku za baadaye katika ulimwengu unaotegemea teknolojia kwa ustawi.
[ad_2]
Source link