Connect with us

General News

Ieleweke kuwa raia hawezi kushiba kwa ahadi tupu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ieleweke kuwa raia hawezi kushiba kwa ahadi tupu – Taifa Leo

TAHARIRI: Ieleweke kuwa raia hawezi kushiba kwa ahadi tupu

NA MHARIRI

KATIKA kila mwaka wa uchaguzi, imekuwa kama desturi bei za bidhaa mbalimbali kupanda kwa kiwango cha kushtua.

Mwaka huu, hali imekuwa mbaya zaidi kwa vile hali ya kiuchumi pia imeathiriwa na matukio mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Matukio kama vile janga la Covid-19 lililotikisa ulimwengu, vita vya Urusi dhidi ya Ukraine na kiangazi kilichodumu kwa muda mrefu tangu mwaka uliopita humu nchini yametajwa kama baadhi ya sababu za changamoto ambazo zinakumba nchi hivi sasa.

Imekuwa vigumu mno kwa wananchi kugharamia mahitaji yao ya kila siku kwa vile matukio haya yote, yakiunganishwa pamoja na kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi, yamesababisha bidhaa muhimu ikiwemo vyakula kuwa ghali mno.

Sasa tumefika katika hali ambapo wateja madukani wameanza kupimiwa viwango vya bidhaa wanavyosahili kununua, iwapo watabahatika kupata bidhaa hizo bado zimo madukani.

Kwa mfano, hivi sasa kuna maduka makuu ambapo wateja hawakubaliwi kununua zaidi ya pakiti mbili za maziwa, sawa na jinsi hawakubaliwi kununua zaidi ya chupa moja ya mafuta ya kupikia iliyopunguzwa bei.

Tunatoa wito kwa wadau wote wanaojali maslahi ya mwananchi wa kawaida kuchukua hatua za dharura ili kuepusha mahangaiko zaidi kwa umma katika siku zijazo.

Taifa hili lilipitia kipindi kigumu mno wakati janga la virusi vya corona lilipokuwa likiangamiza wengi. Wakati huu sasa ingefaa iwe kwamba taifa linashuhudia ufufuzi wa uchumi wake.

Matumaini yaliyokuwa yameanza kuonekana katika ufufuzi wa sekta mbalimbali mwaka huu hayafai kupotelea mbali kwa sababu ya kutojali kwa wadau wakuu wa kimaendeleo, hasa viongozi wa kisiasa.

Huu ni wakati wa kampeni na tunajua ahadi nyingi zitakuwa zikitolewa kwa wananchi, ila ni muda mwafaka kwa viongozi kubainisha uwezo wao na kudhihirisha wanafahamu raia hawezi kula ahadi tupu.

Ikiwa changamoto hizi zote zimeanza kushuhudiwa wakati bado kuna miezi mitano kabla Uchaguzi Mkuu ufanywe, inatia hofu kuwazia jinsi huenda hali ikawa uchaguzi ukizidi kukaribia.

Baadhi ya wataalamu wa kiuchumi huamini kuna waekezaji wa kiviwanda ambao hupunguza shughuli zao za uzalishaji na usafirishaji bidhaa katika kipindi cha uchaguzi wakitazama jinsi hali itakavyokuwa, lakini pia kuna madai kuhusu njama za kusudi za wanasiasa kutatiza biashara wanapotafuta ufadhili wa kampeni.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending