Connect with us

General News

Jamii yataka nayo inufaike kwa mrabaha unaotokana na madini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jamii yataka nayo inufaike kwa mrabaha unaotokana na madini – Taifa Leo

Jamii yataka nayo inufaike kwa mrabaha unaotokana na madini

NA SIAGO CECE

TAKRIBAN wakazi 1,500 waliohamishwa ili kutoa nafasi kwa uchimbaji madini eneo la Kwale, wameitaka serikali iwajumuishe baina ya watakaopokea asilimia 10 ya mrabaha.

Kupitia kwa mwenyekiti wao, Bw Gideon Masyoki, jamii ya Wamaumba Nguluku ilisema iliathirika zaidi na kuwa ya kwanza kuhamishwa wakati uchimbaji madini ya titanium ilipoanzishwa.

Serikali haijawahi kutoa mrahaba kwa jamii zilizoathirika na uchimbaji wa madini hayo, licha ya kampuni husika ya Base Titanium kusema iliwasilisha pesa zinazotakikana kisheria kwa serikali.

Wizara ya Fedha ilisema imepiga hatua katika kuhakikisha jamii zinapokea fedha hizo ambazo hugawanywa kati ya serikali ya kitaifa, kaunti na jamii za maeneo yanayoathiriwa na uchimbaji madini.