Connect with us

General News

Jinsi Spika Justin Muturi alivyosherehekea na akina mama waliojifungua Siku ya Wanawake Duniani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jinsi Spika Justin Muturi alivyosherehekea na akina mama waliojifungua Siku ya Wanawake Duniani – Taifa Leo

Jinsi Spika Justin Muturi alivyosherehekea na akina mama waliojifungua Siku ya Wanawake Duniani

NA WINNIE ONYANDO

SPIKA wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi, Jumanne alisherehekea Siku ya Wanawake Duniani kwa kutenga muda na kuwapongeza wanawake 80 waliojifungua katika hospitali ya Mama Lucy Kibaki jijini Nairobi.

Akizungumza katika hospitali hiyo, Bw Muturi alisema kuwa akina mama ndio vyanzo vya uhai na kwa hivyo wanafaa kupewa heshima duniani.

“Nimefurahi kusherehekea siku ya leo (jana Jumanne) na wanawake 80 waliojifungua katika hospitali hii. Wameleta viongozi 80 watakaoongoza nchi hii katika siku za usoni,” akasema Bw Muturi.

Kadhalika alitoa wito kwa wanawake wajihusishe na masuala ya kisiasa na kuwania nyadhifa mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

“Nawarai akina mama watumie nafasi zilizopo ili kuongoza nchi yetu. Naamini kuwa wana ujuzi hitajika wa kuleta maendeleo nchini,” akasema Bw Muturi.

Kwa upande mwingine, alishutumu kitendo kilichotokea katika barabara ya Wangari Maathai Road na kutoa wito kwa wahudumu wa bodaboda wawe na nidhamu na kuepuka tabia potovu kama hiyo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending