Connect with us

General News

Jinsi unavyoweza kuandaa sandiwichi ukitumia slesi za mkate na mayai – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jinsi unavyoweza kuandaa sandiwichi ukitumia slesi za mkate na mayai – Taifa Leo

MAPISHI KIKWETU: Jinsi unavyoweza kuandaa sandiwichi ukitumia slesi za mkate na mayai

NA MARGARET MAINA

[email protected]

WATU wengi hufurahia kula sandiwichi kama kiamsha kinywa lakini pia ni chakula cha kuliwa wakati wowote.

Ni rahisi kutengeneza na kula pia.

Muda wa kuandaa: Dakika 5

Muda wa mapishi: Dakika 10

Walaji: 2

Vinavyohitajika

  • Slesi 8 za mkate
  • Mayai 3
  • Siagi ya karanga
  • Blueband
  • Chumvi
  • Maziwa vijiko vikubwa vitano
  • Jibini kiasi ya kukwaruza

Maelekezo

Koroga mayai, maziwa na chumvi kiasi.

Weka kikaangio kwenye jiko kisha mimina mafuta kwenye kikaangio.

Mafuta yakishapata moto weka mchanganyiko wa mayai yako na kaanga yaive, ongeza jibini kisha geuza upande wa pili nao uive vyema.

Chukua kipande cha mkate na upake karanga ya siagi na kipande kingine paka Blueband.

Weka yai lako katikati ya vipande vya mkate, kata kipembezoni na sandiwichi yako ipo tayari kuliwa.

Sandiwichi hii yaweza kuliwa na kinywaji chochote chaguo lako.