Connect with us

General News

Jinsi ya kuandaa ‘chipsi’ za mihogo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jinsi ya kuandaa ‘chipsi’ za mihogo – Taifa Leo

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa ‘chipsi’ za mihogo

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MUHOGO ni zao la pili kuwa na wanga mwingi baada ya viazi vitamu.

Muhogo una faida nyingi mwilini na mojawapo ya faida hizo ni kupandisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa.

Mihogo ina virutubisho kama vitamini C, protini, wanga, sukari, vitamini B, madini ya calcium na magnesium.

  • Husaidia katika kupunguza uzani
  • Huboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
  • Husaidia kuboresha afya ya macho.
  • Huipa nguvu miili yetu kwa haraka.

Vinavyohitajika

  • Mihogo 5
  • Mafuta ya kupikia lita 1
  • Chumvi kijiko 1

Maelekezo

Menya mihogo yako na uioshe vizuri.

Chukua kipario na upare mihogo kisha itandaze kwenye sinia. Acha ikauke kwa muda wa saa moja maji yote yaishe.

Weka mafuta ya kupikia kwenye sufuria na uache yapate moto.

Gawa kwa mafungu matatu chipsi zako mbichi.

Weka fungu la kwanza na kuwa makini kwa sababu mafuta huwa yanakuja juu.

Acha chipsi hizo za mihogo zishikane na ziwe na rangi ya kahawia.

Geuza chipsi zako upande wa pili na uache ziive.

Zikiwa tayari, zitoe uweke kwenye chujio zichuje mafuta.

Acha zipoe kisha weka chumvi.

Unaweza kula na pilipili ya unga au chutney, au ukaweka kwenye urojo.

Mihogo kabla ya kukatwa vipande vidogovidogo. PICHA | MARGARET MAINA

Angalizo

Acha chipsi zikauke kabla ya kuzipika; ukiweka mbichi zinanyonya mafuta.

Kuwa makini zisiungue kwani zikiungua zinakua chungu.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending