[ad_1]
KIDIJITALI: Jinsi ya kutumia simu yako kupambana na viwavi
NA LEONARD ONYANGO
WAKULIMA wamepaza sauti wakiitaka serikali kuwasaidia kupambana na viwavi jeshi (Fall Army Worms), ambao wanaendelea kuharibu mazao kote nchini.
Tangu viwavi hao kuingia humu nchini kwa mara ya kwanza mnamo 2017 kupitia mpaka wa Busia kutoka Uganda, wamesambaa katika kaunti zote 47, kwa mujibu wa takwimu za wizara ya Kilimo.
Ili kujua kwamba mazao yako yamevamiwa na viwavi, unaweza kuchunguza majani.
Ukipata majani ya mimea yako yametoboka na kuna wadudu wadogo, hiyo inaweza kuwa dalili kwamba viwavi hao wamevamia shamba lako.
Unaweza kutumia simu yako kupakua apu ambazo zitakusaidia kutambua na kupambana na viwavi.
Miongoni mwa apu hizo ni Fall Armyworm (Faw) app iliyotengenezwa na Shirika la Utafiti wa Mazao na Mimea nchini (Kalro) na Fall Armyworm Monitoring and Early Warning System (Famews) ya Shirika la Chakula Duniani (FAO).
Apu ya Kalro inatoa maelekezo kuhusu namna ya kupambana na wadudu hao mwenyewe huku ukingojea usaidizi kutoka kwa serikali.
Kulingana na Kalro, mkulima anaweza kukusanya na kuharibu mayai ya viwavi kwa kutumia mikono.
Njia nyingine ni kukusanya wadudu hao kutoka kwenye mimea na kuweka kwenye maji ya sabuni. Kunyunyuzia mimea kwa majivu pia kunaweza kuua wadudu hao waharibifu.
“Ikiwa una kemikali za kuua wadudu, nyunyuzia jioni au asubuhi kabla ya viwavi kujificha,” inashauri apu hiyo ya Kalro.
Apu ya Famews pia inawezesha wakulima kutambua mapema viwavi aina ya FAW na kuchukua hatua za kuzuia hasara zaidi inayotokana na uharibifu huo.
Next article
TAARIFA ZA WIKI: Vijana kupokea mafunzo ya uvuvi katika…
[ad_2]
Source link