Connect with us

General News

Jinsi ya kuwaondoa nzi chumbani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jinsi ya kuwaondoa nzi chumbani – Taifa Leo

Jinsi ya kuwaondoa nzi chumbani

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MBU na wadudu wengine wengi, huuma na husababisha mwasho lakini nzi hawaumi ila wanaweza kufanya ukose raha nyumbani.

Kama wadudu wengine wote wa kiangazi, nzi hutukasirisha sana na wakati mwingine pia kwa sababu kuwafukuza inakubidi kutumia dawa na kemikali ambazo zinaweza pia kuwa na madhara kwa afya zetu. Hii ni kabla ya kujua tiba nzuri za asili kuwafukuza.

Nzi ni wadudu wachafu ambao hubeba bakteria mahali wanapokaa.

Kuna tiba nyingi za asili za kuwafukuza nzi lakini sheria nzuri ni kutunza usafi na usafi wa vyumba tofauti nyumbani.

Lifunge begi la taka kwa uangalifu na usiwe na matunda yaliyoiva zaidi chumbani. Kwa viazi na vitunguu, na kwa matunda yote ambayo yanapaswa kuhifadhiwa kwenye hewa ya wazi na sio kwenye jokofu, ushauri ni kuifunika.

Safisha mara kwa mara mapipa na majaa ya taka na usiyaache wazi.

Safisha bakuli za kuwalishia wanyama na uzibadilishwe mara kwa mara: katika mazingira yenye unyevu, bakteria huenea.

Ikiwa unataka kuwa na suluhisho bora wa kuwafukuza inzi, unaweza kutengeneza dawa ya kuua wadudu nyumbani na viungo vya asili ambavyo unavyo kwenye chumba chako cha kulala.

Majani ya mnaanaa

Loweka majani haya kwenye maji kwa siku kadhaa kisha yaweke kwenye chombo cha kunyunyuzia dawa na kila wakati uweke tayari kutumia, kunyunyuziwa katika vyumba wakati nzi wa kwanza anaonekana.

Majani ya basil

Harufu ya basil ni suluhisho bora dhidi ya nzi. Kupanda basil kwenye bustani yako ni njia nzuri ya kuwafukuza nzi, unaweza pia kuipanda kwenye sufuria ndogo jikoni kwako.

Mdalasini

Nzi huchukia harufu ya mdalasini. Ikiwa unataka wawe mbali na nyumba yako, basi unapaswa kutumia air freshener ya mdalasini. Nyumba yako itanukia vizuri, na nzi watakaa mbali kwa sababu hawatakaa nyumbani kwako.