Connect with us

General News

Joylove FC yagonga Gikambura ligi daraja la kwanza – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Na JOHN KIMWERE

Timu ya wasichana ya Joylove FC imedunga Gikambura Starlets bao 1-0 kwenye uzinduzi wa mechi za Ligi ya Central Regional League (CRL) uliofanyika Gikambura Stadium, Kikuyu.

Joylove FC iliyolenga kurejea kushiriki Ligi ya Daraja la Kwanza ilipata bao hilo dakika ya 25 kupitia kombora lililochanjwa na Halima Melisa. ”Nashukuru wenzangu bila kusahau mlinda lango wetu, Sharon Khasandi kwa kazi nzuri aliyofanya,” alisema nahodha wa Joylove,

Beryn Migalusha. Joylove iliyoshushwa ngazi baada ya kutofanya vizuri katika Ligi ya Daraja la Kwanza muhula uliyopita kwenye kipute hicho imepangwa Kundi B linajumuisha timu 12.Mratibu wa mechi za ligi za wanawake, Doreen Nabwire alisema kuwa la Soka ya Kenya (FKF) limepania kuanzisha ligi za wasichana wasiozidi umri wa miaka 13 na 15 kote nchini.

”FKF chini ya uongozi wake, Nick Mwendwa inalenga kuwapa wachezaji wa kike nafasi ya kupalilia talanta zao wakiwa na umri wa chini,” alisema. Katika uzinduzi huo, Nabwire aliandamana na mwenyekiti wa Tawi hilo, Davis Chege walipotoa mpira mmoja kwa timu zote 21 zitakaoshiriki kipute cha msimu huu ambacho kimegawanywa mara mbili Kundi A na B.

”Natamani sana kuona baadhi yenu mkiteuliwa kuchezea timu za taifa katika viwango tofauti,” Chege alisema. Orodha ya timu za Kundi B ambazo zimethibitisha kushiriki inajumuisha: Joylove Academy, Gikambura Queens, Zoe Unify, Limuru Soccer Academy, Galaxy FC, Maraba Queens, Kikuyu Chiksna Magana Flowers FC.

Joylove FC yagonga Gikambura ligi daraja la kwanza – Taifa Leo
Kocha wa Joylove FC, Joyce Achieng akiongea na wacheazaji wake kabla ya kushuka dimbani kukabili wapinzani wao.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending